Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amewataka viongozi wa Halmashauri zote Mkoani Mbeya kutenga maeneo ya michezo ili kujenga viwanja vya michezo ambavyo vitatumika kwaajili ya michezo mbalimbali na kupelekea vipaji vijana kupata ajira kupitia michezo
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya SAMIA MBEYA SUPER CUP yanayofanyika wilayani Chunya na kushirikisha timu nane toka Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya, amesema kama mkoa wamejipanga kuhakikisha kama mkoa unaongeza timu ligi Tanzania na kusema tayari mikakati mbalimbali imeanza kutekelezwa ikiwepo uzinguzi wa jezi za Mbeya city
“Halmashauri zote mkoani Mbeya Tengeni maeneo ya kujenga viwanja vya Michezo na pia tengeni bajeti kwaajili ya michezo kwani mashindano haya ni endelevu na kwakufanya hivyo ni kummunga Mkono mweshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amenesha juhudi za wazi kuziunga mkono timu za Yanga na Simba kwa kutoa pesa kila walipopata goli katika mashindano ya kimataifa”
“Kuna faida katika Mashindano haya kwani wako wachezaji watachaguliwa kwenda ligi mbalimbali Tanzania na hiyo ndo dhamira kuu ya kuibua vipaji toka mitaani lakini pia mashindano yanalenga kuhakikisha timu toka Mkoa wa Mbeya zinaongezekana katika ligi kuu na Tayari mikakati mbalimbali imewekwa ili kuhakikisha Mbeya City iliyoshuka daraja inarudi ligi kuu”
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka kwaniaba ya uongozi wa wilaya ya Chunya amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa Mashindano haya ya Samia Mbeya Super Cup 2023 huku akiahidi wilaya yake ya Chunya kutoa Mshindi wa Kwanza
Mashindano hayo yanashirikisha timu nane kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya huku wilaya ya Chunya (Mwenyeji) ikitoa timu Mbili, Mpaka sasa Timu ya Mbeya jiji inaongoza Kundi lake kwakuwa na alama nne baada ya michezo mitatu wakati kundi B. timu kadhaa zimefungana kwa kuwa na alama mbili (2) na gori moja)
Mashindano hayo yanaendelea leo tarehe 20/7/2023 kwa timu za CHUNYA B Vs MBEYA DC, KYELA DC Vs RUNGWE, MBARALI Vs MBEYA JIJI, CHUNYA DC A Vs BUSOKELO
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Homera akisalimia na viongozi mbalimbali wa serikali, chama Cha Mapinduzi na Viongozi wa Mpira wa Miguu baada ya kuwasili katika uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ulipo Mbugani
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka akitoa salamu Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Wananchi wapenda Michezo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya Samia Mbeya Super Cup 2023 wilayani Chunya
Baadhi ya wananchi wapenda Michezo wakishuhudia kikundi cha Dance chenye jina Waarabu Dnacers wakitoa burudani Mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa Hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Samia Mbeya Super Cup 2023
Timu zikiendelea kupambana ili kuingia kwenye washindi watatu bora ambao wataensda kushiriki mashindano mengine wilayani Kyela pamoja na kupata zawadi mbalimbali za Samia Mbeya Super Cuyp 2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.