Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Z. Homera amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Chunya kuhakikisha anasimamia suala la misitu kuto kuingiliwa na wachimbaji na kuwataka wanaochimba maeneo ya msitu kuacha mara moja kwani utunzaji wa mistitu ni kwaajili ya manufaa ya sasa na baadae
Maagizo hayo ameyatoa tarehe 8/11/2023 wakati wa ziara yake alipotembelea kituo cha afya cha Sangambi pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo kupitia mkutano wa Hadhara ulifanyika katika viwanja vya sokoni karibu na Ofisi ya Kijiji cha Sangambi .
“Mkuu wa Wilaya simamia suala la msitu ni marufuku mtu kuingia kuchimba eneo la misitu leo hii tumejenga shule na kituo cha afya kwasababu wenzetu walitunza huu msitu kwani kwa kuchimba eneo la msitu mtaacha mashimo na wanafunzi watakosa maeneo ya kujifunzia” alisema Mhe. Homera
Aidha Mhe Homera amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Mbeya kuhakikisha umeme unapatikana kwenye kituo cha Afya Sangambi huku akimpa muda wa mwezi mmoja kutekeleza agizo hilo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi wanaoenda kupata huduma katika kituo hicho
‘’Maagizo haya nampa meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya wekeni mpango wa dharula hapa hakikisheni umeme unapatikana katika kituo hiki cha afya cha Sangambi ndani ya mwezi mmoja tunajua kuna changamoto ya vifaa lakini umeme lazima upatikane “aliongeza Mhe. Homera.
Akitoa salam za Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mayeka S.Mayeka amesema kuwa Wilaya ya Chunya amesema wilaya ya Chunya inakua kwa kasi hivyo amewataka wananchi kupitia serikali za vitongoji na vijiji kuzingatia mpango mzuri wa ujenzi jambo litakalofanya mitaa na vijiji kuwa na barabara zinazopitika pamoja na mpango mzuri wa makazi pasina kusubiri serikali kuja kusimamia zoezi hilo
Awali akisoma taarifa ya kituo cha afya cha Sangambi afisa elimu kata Mwalimu Joseph Kihwele amesema katika utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa kituo cha afya kumekuwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni kukosekana kwa umeme katika kituo hicho cha Afya pamoja na mabadiliko ya gharama za vifaa vya ujenzi.
Adam Mwakalobo, Frank Mbwilo na wengine walitoa kero zao juu ya namna serikali za vijiji zinavyopendelea baadhi ya watu kugawa maeneo ya msitu kwaajili ya machimbo jambo ambalo limepelekea mkuu wa Mkoa kupiga marufuku uchimbaji ndani ya misitu hiyo, kero nyingine zilizopatiwa majibu ni pamoja na suala la maji, Barabara na nyingine nyingi
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Wilayani Chunya Imedumu kwa siku tatu kuanzi tarehe 6/11/2023 na kuhitimisha tarehe 8/11/2023 ambapo amekagua miradi mbalimbali yya maendeleo, misitu ya Hifadhi pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia majibu. Ziara hiyo imehusisha kamati ya ulinzi na usalama Mkoa na wilaya na, wataalamu mbalimbali kutoka Mkoani na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya , wakuu wa taasisi mbalimbali na Waandishi wa Habari.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mayeka S. Mayeka akitoa salam katika kituo cha Afya cha Sangambi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa walipotembelea na kukagua kituo hicho.
.Akisoma taarifa fupi ya mradi wa kituo cha Afya cha Sangambi wakiti wa ziara ya Mkuu wa Mkowa wa Mbeya Mhe.Juma Z.Homera
Adam Mwakalobo mkazi wa kijiji cha Sangambi akitoa kero yake mbele ya Mkuu wa Mkoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Sokoni kijiji cha Sangambi
`
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.