Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amesema wilaya ya Chunya itabadilika sana katika Nyanja mbalimbali ikiwepo miundombinu ya barabara kutokana na miradi inayotarajiwa kutekelezwa wilayani humo kwani wawekezaji mbalimbali wako tayari kuwekeza katika wilaya hiyo jambo ambalo litaongeza mzunguko wa fedha na kuketa maendeleo
Mhe. Homera ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya chunya cha kujadili na kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali CAG
Mhe Homera amewataka viongozi wilayani Chunya kuendelea kuwa na umoja na mshikamano katika utekelezaji wa Majuku yao kwani palipo na migogoro hapawezi kupata maendeleo, Migogoro sio sehemu ya serikali ya awamu ya sita na haileti maendeleo kwa Taifa
“Tunakwenda kuanza utekelezaji wa ile fursa ya uwekezaji katika kata za Nkung’ungu na Lupa,ule uwekezaji ni Mkubwa Kampuni ziko tayari kufanya uwekezaji hivyo barabara zitatengenezwa, Chunya itakuwa ni wilaya ya Uchumi Mkubwa mkoani Mbeya, Hivyo endeleeni kuwa wamoja kwani Migogoro haina nafasi”
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Rodrick Mpogole akizungumza katika kikao hicho, amewataka watumishi kuhakikisha wanazuia hoja za ukaguzi na pale inapojitokeza hoja ya mkaguzi ni lazima ijibiwe kwa ufasaha, aidha tufanya kazi kwa ufasaha na ufanisi ikiwa ni njia bora na sahihi ya kuzuia hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali
“Kwaniaba ya watumishi naomba niseme mambo matatu kwanza vikao hivi si vizuri sana na vinapotokea ni kwamba sisi watumishi tunashida hivyo tutengeneze mkakati wa kuzuia hoja za ukaguzi na pale ambapo hoja za ukaguzi zimejitokeza ni lazima zijibiwe kwa wakati na jambo la tatu naomba tufanye kazi kwa umakini na ufanisi kama njia ya kuzuia hoja za ukaguzi” amesema Mpogole
Nae mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Simaon Mayeka akitoa salamu za serikali wilayani Chunya, amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kikao hicho na amesema maelekezo yote kwa mujibu wa kikao yatatekelezwa kwa ufanisi mkubwa, aidha amesisitiza watumishi kuandaa taarifa sahihi na kwa umakini mzuri ili kuepuka kupoteza muda bila sababu
“Naomba nitoe ushauri kidogo, watumishi mnapoandika taarifa ziandikwe kwa umakini ili kuepuka usumbufu na kupoteza muda bila sababu Mfano kama Kituo cha Afya mtande hoja inaeleza kutokuwepo kwa Mbao wakati Mbao zililetwa na zimetumika kujenga na tayari kituo kinafanya kazi kwahiyo niwaombe mjitahidi kuweka vizuri taarifa zenu ili kuepuka kupoteza muda”
Naye Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona amesema Mpaka sasa halmashauri ya wilaya ya Chunya ina asilimia tisini (90%) ya ukusanyaji wa mapato na bila shaka wanaongoza katika Mkoa na lengo sio kuongoza kwenye mapato peke yake bali na maeneo mengine mengi na sababu ya kuongoza kwao ni ushirikiano mzuri kati ya ofisi ya Mkuu wa wilaya na ofisi ya Mkurugenzi lakini pia usimizi mzuri wanaoupata kutoka kwa baraza la madiwani likiongozwa na Mwenyekiti wake makini Mhe Bosco Mwanginde ambaye ni Diwani wa kata ya Mbugani
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde wakati akihitimisha kikao hicho amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kwa busara, hekima na utulivu wakati wa kikao hicho muhimu cha kujadili hoja za mkaguzi wa Hesabu za Serikali katika halmashauri ya wilaya ya Chunya
Aidha Mweshimiwa Mwanginde amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba baraza la madiwani wilayani Chunya wataendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chunya itaendelea kuongoza katika Nyanja zote katika mkoa wa Mbeya na hatimaye Taifa kwa ujumla
Baraza hilo la Madiwa liliketi tarehe 10/03/2023 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) Lengo likiwa kujadili hoja mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali zilizotokana na ukaguzi maalumu ulifanyika hivi karibuni na kufanyia kazi mapendekezo ya Ofisi ya CAG
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde akizungumza katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani lililoketi Machi 10 kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.