Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Chunya kwa matumizi mazuri ya mapato ya ndani katika ujenzi wa miradi ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Stend mpaya ya Mabasi itakayojengwa Kijiji cha Sinjilili katika kata ya Itewe .
Pongezi hizo amezitoa Septemba 9, 2024 wakati wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Wilaya ya Chunya ambayo inajengwa na mkandarasi mzawa (AMJ Global Mult Constractors Company kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Tunajivunia Wilaya ya Chunya kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi sahihi ya mapato hayo kwani mmejenga miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri.” alisema Homera.
Homera, ameweka bayana dhamira ya Mhe. Rais juu ya matumizi sahihi ya mapato ya ndani pamoja na kuhakikisha miradi ya maendeleo inajengwa na kukamilika kwa wakati .
Naye Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga amemhakikishia Mhe.Homera kwamba watasimamia ujenzi wa stendi hiyo ya mabasi inayotarajiwa kuanza kujengwa ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliokusudiwa na kwa viwango.
Aidha , Mhe. Batenga amesema Wilaya ya Chunya ni Wilaya ya madude (majengo) na wananchi wake wamekuwa wakijituma na kuchangia shughuli mbalimbali za Maendeleo ili kuungana na Serikali kuhakikisha wananchi wake wakiwepo wananchi wa wilaya ya Chunya wanapata Mendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Mhe. Bosco Mwanginde wakati akitoa salamu za wananchi kwa Mkuu wa mkoa amesema yeye na baraza lake kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri watahakikisha wanasimamia ujenzi huo kwa weledi na kuhakikisha muda waliokubaliana na mkandarasi kukamilisha ujenzi unazingatiwa na mradi unakamilika kwa viwango vilivopo kwenye mkataba.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa stendi hiyo ya mabasi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona amesema, mradi huo utagharimu kiasi cha Bilion 3.1 ambazo ni mapato ya ndani ya Halmashauri.
“Stendi hii ni maagizo ya Mheshimiwa Rais alipokuja Chunya mwaka 2022, aliagiza Halmashauri ijenge stendi kupitia mapato yake ya ndani” alisema Kambona.
Hafla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Stend mpya ya Mabasi Chunya imefanyika tarehe 9/9/2024 katika viwanja ambapo stendi hiyo itajengwa na imeshuhudiwa na kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Mbeya, Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya, Viongozi wa dini, viongozi wa mila ,Wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri, wandishi wa Habari, wakuu wa Taasisi, Wadau wa Maendeleo na Wananchi wa wilaya ya Chunya Hususani wananchi wa kata ya Itewe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Alikaa upande wa Kulia na amevaa koti la draft na Tishert ya njano Ndani) akisaini mkataba wa ujenzi wa Stendi ya Mabasi wilaya ya Chunya, Upande wake wa pili ndiye Mkandalasi wakati upande wake wa Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Baadhi ya waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakishuhudia zoezi la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Stendi Mpya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.