Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mbe. Juma Zuberi Homera amesema Serikali ya awamu ya sita ina lenga kumkwamua mwananchi wa chini akiwepo mkulima wa zao la Tumbaku ndio sababu inahakikisha soko la Tumbaku linasimamiwa ipasavyo jambo ambalo limeleta faraja kwa wakulima katika msimu wa kilimo wa mwaka 2022/2023 ambapo bei ya Tumbaku katika mkoa wa Kitumbaku Chunya ni dola 2.42 huku wastani wa bei nchini ikiwa ni dola 2.0
Akizungmza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa masoko ya Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Chunya katika Chama cha msingi Mtanila Mhe Homera amewapongeza wakulima wa tumbaku kwanza kwa namna wanavyoshiriki katika kilimo lakini pia amewataka viongozi kuendelea kuwasimamia wakulima katika maeneo mbalimbali ili uzalishaji wao uwe wenye tija
“Bei nilizoziona ni nzuri sana na nimpongeze sana mnuzi kwa bei hizi, lakini pia niwapongeze wanamtanila kwasababu wameandaa vizuri sana Tumbaku kasoro hizi chache zisitufanye turudi nyuma bali tuzirekebishe na tusonge mbele lakini nimeona viongozi wa chama hiki wako smati na muendelee kuwasimamia vizuri wakulima ili waendelee kuzalisha kwa tija, Msione bei inachangamka namna hii Mhe Rais ameona Zao la Tumbaku liwe zao la kumkwamua Mwananchi”
Aidha Mkuu wa Mkoa amezindua rasmi ghala la Chama cha Msingi Mtanila lenye uwezo wa kubeba mituma 2500 kwa wakati mmoja lenye thamani ya milioni 200 pia amekabidhi trekta lenye thamani ya milioni 73 kwa chama cha Msingi Mtanila na baadaye amewakabidhi pikipiki za magurudumu matatu (Guta) wakulima kumi baada ya kupata Mkopo kutoka Banki ya Azania
“Vyama vichache sana vinanunua vyombo kama hivi, wangekuwa wengine wangepiga dili, wangesema trekta hili limenunuliwa kwa milioni 100 lakini ninyi mmeenda kwenye uhalisia milioni 73 zimetumika hongereni sana, muendelee hihivi na mwakani muongeze trekta linguine, hongereni sana Mtanila”
Meneja wa Banki ya Azania Ndugu Samson Basil Mahimbi amesema wao kama wadau wa kilimo wataendelea kutoa mikopo kwa riba nafuu kwa wakulima ikiwa ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inalenga kuwaletea wananchi wake Maendeleo
“Mtanila ni miongozi mwa vyama saba ambavyo msimu uliopita tumewakopesha zaidi ya dola milioni saba na nusu sawa na bilioni 17 na wakulima zaidi ya 3000 wamenufaika na mikopo toka Azania kwa asilimia saba na mwakani tutaendelea kufanya hivyo ili tunaposema Azania Benki ni bega kwa began a wakulima huwa tuna maanisha kweli”
Awali aikitoa taarifa kwa mgani rasmi, viongozi wa serikali, taasisi za serikali na binafsi pamoja na wananchi waliojitokeza Mhasibu Mkuu wa Chama cha Msingi cha Mtanila Ndugu SEIF MARIJANI amesema chama kimefanikiwa maeneo mbalimbali huku akitaja changamoto ya Mbolea kukwamisha maendeleo ya kilimo.
“Chama cha Msingi Mtanila kimefanikiwa kujenga ghala la kuhifadhia tumbaku lenye uwezo wa kuhifadhi mitumba 2500 kwa wakati mmoja, tumefanikiwa kunua trekta kwa gharama ya milioni 73 kupitia mapato ya ndani, chama kina mfuko wa pembejeo, kujenga ofisi ya Chama, kuandaa shamba la miti ambalo limepandwa miti laki moja mwaka 2023 lakini tunazo changamoto ya pembejeo za kilimo tofauti na misimu mingine iliyopita”
Hafla ya ufunguzi rasmi wa masoko ya Tumbaku katika Mkoa wa Kitumbaku Chunya imefanyika tarehe 17/5/2023 katika kata ya Mtanila ambapo Chama cha Msingi Mtanila kilikuwa mwenyeji kwa niaba ya vyama vingine 27 ambapo shughuli mbalimbali zilifanyikiwa ikiwepo uzinduzi wa ghala, kukabidhi trekta, pamoja na kukabidhi pikipiki za Magurudumu Matatu kwa wakulima kumi ambapo banki ya Azania imewakopesha wakulima hao.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera akizindua Ghala la kuifadhia Tumbaku chama cha Msingi Mtanila
Muonekano wa Ghala la Kuifadhia Tumbaku Chama cha Msingi Mtanila
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.