Afisa Elimu awali na Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu ferd Y Mhanze ameawata wanafunzi wa sekondari wilaya ya Chunya kuongeza juhudi za kujifunza Lugha ya kingereza kwani itawarahishia kujibu mitihani yao ya kidato cha pili inayowakabili lakini pia itawapa uwezo wa kujieleza katika ulimwengu huu wa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia
Ametoa kauli hiyo mapema leo wakati alipopata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Bitimanyanga iliyoko kata ya Mafyeko wakati wa ziara ya kamati ya Fedha Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya
“Ongezeni juhudi sana katika kujifunza Lugha ya kingereza maana ndiyo Lugha inayotumiwa kuwatahini na hata katika mawasiliano mbalimbali ya kimataifa hutumika Lugha ya Kingereza na msipofanya hivyo maana yake mmeamua kufeli maana masomo yote isipokuwa somo la Kiswahili pekee ndilo mnajifunza kwa Kiswahili na mtatahiniwa kwa Lugha ya Kiswahili”
Aidha Mwalim Mhanze amewataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa waliyoipata ya kusoma katika kipindi ambacho serikali imeboresha mazingira ya kusomea bila kujali jiografia ikiwa ni pamoja na uwepo wa Maabara za fizikia. Kemia na baiolojia kwenye shule za sasa ni tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani.
“Ninyi mna bahati sana ila mnashindwa kuitumia, serikali inaleta fedha nyingi na nyinyi ni mashahidi, leo maktaba, maabara zinajengwa hivyo mnasoma hata kwa vitendo moja kwa moja, sisi wenzenu tulipokuwa tnasoma tulisoma “Luminous frame” lakini hatukuona hiyo “luminous frame” kwa macho maana “Bansen Barner” Hazikuwepo lakini ninyi mnasoma Darasani na baadaye mnaenda maabara kuona kile alichofundishwa mwalimu, Hiyo ni fursa itumieni” Amesema Mwalimu Mhanze
Naye afisa Elimu wa sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu Hamis Mapoto alipata nafasi ya kuungana na Mwalimu Mhanze Darasani baada ya kukamilisha ukaguzi wa mradi wa matundu sita ya vyoo na ukarabati wa madarasa mawili ambapo amewambia wanafunzi hao kwamba wao wamepata bahati ya kutembelewa na viongozi wakubwa hivyo iwe chachu kwao katika masomo yao
Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzao wa kidato cha pili wa Elika Samson Briyton, Maimuna John Kawila na Clever Yonifat Mbuza wamesema sababu kubwa inayopelekea wanafunzi wengine kufeli ni uvivu wa kusoma hivyo wao wamewaahidi viongozi waliowatembelea kusoma kwa bidii na kujituma ili kumtendea haki Mhe Rais anayepeleke fedha za kujenga na kuendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo
Shule ya sekondari Bitimanyanga imepewa fedha shilingi milioni 31 ili kukamilisha madarasa mawili ambayo yalikuwa maboma na kujenga matundu sita ya vyoo ikiwa ni juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Mwalimu Mhanze akiwa anaeleza jambo wakati alipokuwa anazungumza na wanafunzi wa kidato cha Pili Shule ya Sekondari BitiManyanga
Mwalimu Mhanze akiwa darasani na katika picha ishara hiyo alikuwa anasisitiza umuhimu wa kiingereza kufikia ndoto zako za Mbeleni
Bado kwa msisitizo mkubwa Mwalimu Mhanze akionesha ishara mbalimbali huku akisisitiza umuhimu wa kusoma kwa bidii huku mkazo ukiwa kwenye Lugha ya Kiingereza
Mwanafunzi Elika Samson Brayton wa shule ya sekondari Bitimanyanga kidato cha Pili akijibu swali wakati wakipewa maelekezo na Mwalimu Mhanze
Mwanafunzi Clever Yonifat Mbuza akijibu swali aliloulizwa na Mwalimu Mhanze wakati akizungumza na wanafunzi hao kuhusu umuhimu wa kituma kujifunza Lugha ya Kiingereza
Wanafunzi wa kidato cha pili wakiwa wanasikiliza kwa umakini maelekezo na kwa Mbali mwanafunzi Maimuna John Kawili amenyoosha mkono akionesha anataka kuuliza jambo kwa mwalimu Mhanze ili kufikia ndoto zake
Afisa elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu Hamis Mapoto akizungumza Jambo na wanafunzi wa kidato cha pili baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi wa miradi chini ya kamati ya fedha, uchumi na mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.