Afisa lishe Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala ametoa rai kwa wanafunzi kuzingatia masuala ya lishe kwani jinsi mtu anavyoonekana leo inategemea na vyakula ambavyo mtu anakula hivyo mtu kuwa na mwonekano mzuri na wenye afya anapaswa kuzingatia mlo kamili ukiambatana na makundi mbalimbali ya vyakula.
Kauli hiyo amezungumza leo Octoba 10/2024 wakati akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe ikiwa ni pamoja na kufundisha makundi mbalimbali ya chakula kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makala iliyopo Kata ya Matundasi Wilaya ya Chunya.
“Niwaombe wanafunzi mzingatie sana masuala ya lishe kwani lishe ni muhimu sana kwenu ikiwemo protini kwani inaujenga mwili lakini hiyo hiyo protini ndani yake kuna mafuta ambayo yanatunza kumbukumbu na utengenezaji wa ubongo hivyo wazazi wakati mwingine wanaponunua maziwa tuwe tunakunywa ili akili iweze kuchangamka” . alisema Mayala
Aidha Afisa lishe ameelezea makundi mbalimbali ya vyakula kama vile nafaka , mizizi, vyakula jamii ya mikunde, wanyama ,mafuta , Mboga mboga na matunda pamoja na umuhimu wake ikiwa ni pamoja na kuulinda mwili dhidi ya magonjwa kuupa mwili nguvu na afya pamoja na mambo mengine mengi huku akisisitiza kujiepusha kula vyakula vyenye kemikali nyingi.
Naye Afisa elimu Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo maalumu divisheni ya elimu Sekondari Mwalimu Lukelo Mng’ongo amewataka wanafunzi kuyazingatia masuala ya lishe ambayo wamefundishwa lakini pia kwendelea kusoma kwa bidii Zaidi huku akitoa rai kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwendelea kujiandaa vyema na mtihani wa taifa ulioko mbele yao.
Maadhimisho ya wiki ya lishe yameambatana na utoaji elimu juu ya mambo mbalimbali kuhusiana na lishe kwa wanafunzi ili kuwawezesha kujua na kutambua umuhimu wa lishe na jinsi ya kuzingatia lishe bora kwa afya zao imeenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Mchongo ni afya yako, Zingatia Unachokula”.
Afisa elimu Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo maalumu divisheni ya elimu Sekondari Mwalimu Lukelo Mng’ongo akitoa rai kwa wanafunzi kuongeza bidii zaidi katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani iliyoko mbele yao.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makala kata ya Matundasi wakiendelea kufuatilia elimu ya Lishe
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.