Mwenge wa uhuru umezindua, umetembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 wilayani chunya.
Akizungumza katika maeneo ya miradi, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Sahili Nyanzabara amewataka wataalam wa ujenzi kufuata miongozo iliyowekwa na wizara wakati wa utekelezaji wa shughuli za ujenzi wa miradi ili kuepuka kufanya kazi chini ya kiwango ama kinyume na miongozo hiyo
Nyanzabara amesema kutofuata maelekezo yaliyotolewa katika miongozo ni jambo ambalo halipaswi kuendelea kutokea, watalamu na watendaji wetu hakikisheni mnafuata taratibu na Miongozo iliyotolewa.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru mwaka 2022 katika wilaya ya chunya ni Ujenzi wa zahanati ya Ituma, Ujenzi wa madarasa mawili na Ofisi shule ya Sekondari Isenyela , Mradi wa maji Sangambi, Kikundi cha Vijana cha Sabasaba, Ujenzi wa daraja la Nselewe Kata ya Chokaa pamoja na Ujenzi wa kiwanda cha Kuchakata dhahabu,
Kwaupande wa mkuu wa Wilaya ya Mh. Mayeka S. Mayeka amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa na kumshukuru kwa kukubali kuizindua miradi ,
Aidha Mayeka ameahidi kuyafanyia kazi mara moja maelekezo yote yaliyotolewa na Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru.
Mhe Mayeka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo, ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Naye Mbunge wa jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka amewapongeza wataalam kwa kazi nzuri wanayofanya katika kutekeleza miradi na kusisitiza matumizi mazuri ya rasilimali fedha zinazolewa na Serikali kwa manufaa ya umma.
Nyanzabara ametumia fursa hiyo kukemea vitendo vya rushwa,ameawakumbusha wananchi kuzingatia mlo kamili,kujikinga na malaria na kukemea vikali matumizi ya dawa za kulevya.
“ Mama zangu mliyopewa vyandarua hakikisheni mnavitumia vyandarua hivyo kulingana na maelekezo mliyopewa na wataalamu tumieni kwa usahihi, wapo wengine wanapewa vyandarua wanaenda kufunikia vifaranga, bustani na hata kuvulia samaki hayo sio matumizi sahihi ya vyandarua” Nyanzabara
Pia amewapongeza wananchi wa wilaya ya chunya kwa uzalendo wao na kujitoa katika kushiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Ndugu Sahili Nyanzabara wa katikati kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa akiwa na Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh. Mayeka Mayeka upande wa kushoto sambamba na Mkurrugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona upande wa kulia katika moja ya mradi uliyozinduliwa na mwenge wa Uhuru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona wakwanza kulia akitoa maelezo kwa kiongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara katika moja ya Mradi uliyotembelewa na mwenge wa uhuru
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.