Mwenge wa uhuru mwaka 2023 unataraji kukimbizwa Kilometa 1155.5 katika halmashauri zote saba za Mkoa wa Mbeya na utadumu kwa siku saba ambapo miradi yenye Thamani ya Bilioni 36.4 itatembelewa, itazinduliwa na mingine itawekewa mawe ya msingi
Akizungumza katika hafla ya mapokezi ya mwenge kimkoa 7/9/2023 katika kijiji cha Ikuti halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Mbeya utakimbizwa umbali wa kilometa 1155.5, miradi mbalimbali itatembelewa, kuzinduliwa na kuweka mawe ya msingi katika miradi 45 yenye thamani ya 36.4
Mwenge wa uhuru September 7, 2023 unakimbizwa wilayani Rungwe kwa umbali wa kilometa 100 huku mkesha ukitajwa kufanyika uwanja wa shule ya Msingi Kiwira iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe na kesho utakabidhiwa katika wilaya ya Kyela na kuendelea kukimbizwa huku na baadaye Halmashauri nyingine za Mkoa wa Mbeya
Wilaya ya Chunya inataraji kupokea Mwenge wa Uhuru Septemba 13,2023 katika uwanja wa Mpira wa Miguu Sinjilili na kukumbizwa kilometa 247 ambapo mwenge utembelea, utazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye Miradi yenye thamani ya bilioni 2.9 huku mkesha wa Mwenge wa uhuru 2023 wilayani Chunya ukitaraji kufanyika kijiji cha Bitimanyanga.
Miradi mbalimbali ikiwepo Mradi wa ujenzi wa shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza wenye thamani ya Milioni 348, Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya wilaya ya Chunya wenye thamani ya milioni 384, mradi wa zahanati ya Everest wenye thamani ya Milioni 48, ujenzi wa maabara ya kupima madini ya dhahabu wenye thamani ya milioni 955, Mradi wa uchimbaji visima 26 wenye thamani ya milioni 910 na ujenzi wa kiwanda kidogo cha kusindika mafuta na kusaga unga wa mahindi wenye thamani ya milioni 263
Mwenge wa uhuru 2023 umepokelewa 7/9/2023 katika Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa wilaya ya Mbeya akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbyea ukitokea katika Mkoa wa Songwe ambapo Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bi Ester Mahawe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo amekabidhi mwenge wa uhuru 2023 baada ya kutamatisha ratiba yake ya kuangazia, kumulika, kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya mkoa wa Songwe
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika hafla ya mapokezi ya mwenge kimkoa wilayani Rungwe
Mwenyekiti wa umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Chunya mdugu Leckson O. Mwakasuluka ( wapili kutoka kulia waliovaa kombati) ni moja kati ya wakimbiza mwenge ngazi ya Mkoa katika haflea ya mapokezi ya mwenge kimkoa iliyofanyika wilayani Rungwe katika kijiji cha Ikuti
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.