LUALAJE
MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kutunza, kulinda na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili idumu kwa muda mrefu na hatimaye kuwanufaisha watu wengine wengi.
Mhe. Mwanginde amesema hayo jana tarehe 20 January 2023 wakati alipoongoza hafla ya ufunguzi wa shule ya Sekondari Lualaje ambayo imejengwa kwa fedha kiasi cha Shilingi milioni 470 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi wote bila kujali eneo analotoka
Aidha Mhe Mwanginde amewasisitizia wananchi wa lualaje kwamba Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan inawajali na inawatambua na ndio sababu inaendelea kuleta maendeleo mbalimbali ikiwepo ujenzi wa sekondari inayofunguliwa, miundombinu ya Barabara, vituo vya afya pamoja na miradi mbalimbali.
“Kuletwa kwa fedha katika kata hii ya Lualaje ni ishara tosha kwamba serikali inawajali, na inawathamini sana wananchi wake, na ufunguzi wa shule hii ni mwanzo kwani iko miradi mingine mingi serikali inaendelea kutekeleza katika maeneo yenu”
Katika kuhitimisha Hotuba yake katika hafla hiyo amewata wanafunzi, walimu na wazazi kwa pamoja kushirikiana ili kuhakikisha lengo la uwepo wa shule ya sekondari katika maeneo yao linatimia kwani kinyume na hapo itakuwa ni vigumu kupata matokeo chanya kwa wanafuniz na serikali kwa ujumla.
Pia Mhe Mwanginde amewaagiza watendaji wote kata na vijiji wilayani chunya kuanza kuchukua hatua mara moja kwa wazazi ambao bado hawaja wapeleka watoto shuleni na kuwataka kupeleka taarifa ofisini kwake mara moja.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona amewapongeza wananchi wa kata ya Lualaje kwa namna walivyoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo ya sekondari na kuwataka kutunza, kulinda na kuhakikisha wanaendelea kushiriki katika miradi mingine mingi inayojengwa katika maeneo yao
Naye Afisa Elimu sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalimu Hamis Mapoto alitoa takwimu za wanafunzi waliopangwa katika shule hiyo ya Sekondari Lualaje ni wanafunzi 86, aidha ni wanafunzi 61 tu wamesharipoti shuleni hapo huku akisema tayari walimu saba wamepelekwa katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya chunya Mhe. Bosco Mwanginde akikata utepe kuzindua majengo ya Shule ya Sekondari Lualaje.
Muonekano wa Majengo Katika Shule ya Sekondari Lualaje
Wanafunzi sambamba na wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya Uzinduzi wa Shule ya Sekondari Lualaje
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Shule ya Sekondari Lualaje.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.