Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka viongozi kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, miongozo na sheria zilizopo.
Mwanginde ameyasema hayo ameyasema leo Agosti19, 2022 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasiliana na kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka 2021/2022, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Chunya {Sapanjo Hall}.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Mwangine amesisitiza viongozi wanapaswa kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, miongozo kanuni na sheria zilizopo ili kufanya kazi kwa ufanisi na uadilifu na kuleta tija katika kushughulikia wananchi.
“Kwa kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yetu kila mmoja wetu kwa nafasi yake na taaluma yake afanye kazi kwa uadilifu na kuhakikisha kwamba wananchi ambao waliotupa dhamana wanapata huduma iliyo bora na stahiki." Alisema Mwanginde.
Vilevile aliwasisitizia viongozi na wataalam kuhakikisha wanaendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi {CCM} ya miaka mitano 2020/2025 ili kutenda haki nakutimiza ahadi na miongozo ya chama hicho.
Mwanginde aliongeza kwa kusema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imepokea jumla ya shilingi bilioni 5.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya na utawala ambapo miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali katika maeneo yanayosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya hiyo imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani jumla ya shilingi bilioni 5 na kushika nafasi ya pili kimkoa katika ukusanyaji wa mapato.
“Mabadiliko haya katika makusanyo yetu ya ndani yametupa faraja kubwa sisi kama viongozi wenye dhamana ya kazi hiyo, lakini pia imetoa faraja kwa watendaji wetu ambao ndio wasimamizi wa shughuli ambazo tumewakabidhi."Alisema Mwanginde.
Aidha Mwanginde ametoa rai kwa viongozi na wataalam kuendelea kushirikiana kwa hali na mali katika kuendelea kutekeleza hayo ili kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Chunya inakusanya mapato kwa kiwango ambacho kipo kwenye bajeti na kuweza kufanikisha yale yote ambayo yamewekwa kwenye bajeti hasa miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.