Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde leo 20 December 2022 amekabidhi pikipiki 13 kwa Watendaji wa kata zenye thamani ya shilingi milioni 36.1, kwa ajilia ya kuwasaidai katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato, usimamizi wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha Halmashauri inafikia lengo walilojiwekea kwenye ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo Mwanginde amesema lengo la kuwapa pikipiki ni kuwarahisishia watendaji kwenda kukusanya mapato na kusimamia miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao ya kazi.
Pia Mwanginde ameipongeza halmashauri kwa kutenga fedha na kununua vitendea kazi hivyo kwa maafisa watendaji kwani zitawarahishishia kufika katika maeneo yao ya kwazi wa wakati na kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato.
“Ndugu zangu hizi pikipiki kazi yake kubwa ni kukusanya mapato na kuleta mapato halmashauri ili yaingie kwenye utaratibu wa matumizi” amesema Mwanginde
Mwandinde ametoa wito kwa watendaji wote waliokabidhiwa pikipiki hizo kwenda kuzitumia kwa shughuli zilizokusudiwa na sio vinginevyo na kuwa hatamfumbia macho mtendaji yeyote atakaye badilisha matumizi ya pikipiki hizo.
Hata hivyo Mhe Mwanginde amewaasa na kuwataka watendaji kuwa makini sana na pikipiki hizo kwani wizi wa pikipiki umeshamiri sana hivyo wanapaswa kuzituna na kuwa makini nazo.
Matukio mbalimbali katika pichaMwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde akizungumza jambo kabla ya kuwakabidhi watendaji wa kata pikipiki
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.