Halmashauri ya wilaya ya Chunya imepokea mradi wa kuwawezesha vijana kujitambua “KIJANA WA MFANO” ambao utatekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya YOUNG & ALIVE INITIATIVE (YAI) ambapo kata sita za wilaya ya Chunya zitafikiwa na mradi huo.
Mradi huo unalenga kuzifikia Kata za Itewe, Chokaa, Makongolosi, Bwawani, Matundasi na Chalangwa.
Akizungumza katika kikao cha kuutambulisha Mradi huo kilichoshirikisha Wataalamu kutoka idara Mbalimbali za Halmashauri ya wilaya ya Chunya katika ukumbi wa Mikutano jengo jipya la Halmashauri , Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo Ndugu William Otuck amesema lengo la Mradi huo ni kuwajengea uwezo vijana katika mambo mbalimbali yakiwepo Namna ya kuzuia Ukatili, Uelewa wa Masuala ya Fedha, Uelewa juu ya Madhara ya Pombe na Madawa ya Kulevya, Uelewa juu ya Masuala ya Uzazi na Mambo mengine
Katibu Tawala wa wilaya ya Chunya Bw. Anakletth Michombero ameshauri mradi huo uwafikie vijana wa Chunya kwa uwakilishi wao huku akihoji sababu zilizotumika kuchagua kata tajwa hapo juu huku akisema zote zinakaribia katika mambo mengi hasa shughuli za Kiuchumi (Uchimbaji) Jambo ambalo linaweza kushindwa kuleta ufanisi kwani jamii nyingine kama za kifugaji na kilimo zimeachwa kando.
“Ningeshauri huu mradi ungehusisha jamii za kifugaji na hata za wakulima kwani nazo zimesikika sana katika mambo ya ukatili wa kijinsia na mambo mengine hivyo mradi ungewahusu katika kuleta ustawi wa wanajamii na Taifa kwa ujumla wake” Michombero
Mratibu wa Afya ya Uzazi wilaya ya Chunya Bi Nerea Mwafulilwa amehoji namna ambavyo mradi wa “Kijana wa Mfano” utakavyo wafikia watu wengine ambao ni sheheumu kubwa ya jamii ambako vijana lengwa wanakotoka ili hali mradi unawahusu vijana pekee
James Masunge na Grolia Kavishe kutoka ofisi ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Chunya, Zabron Mwalyego kutoka ofisi ya Ustawi wa Jamii Chunya, Cutherbth Mwinuka kutoka ofisi ya Kilimo Chunya, pajoa na wadau wengine wamehoji sababu za Mradi kutohusisha kilimo kwa sasa, Mbinu watakazotumia kuhakikisha ushiriki wa Vijana unakuwa wa kutosha lakini pia tija ya mradi kwa ujumla wake na baadaye kutoa mapendekezo mbalimbali ili kuboresha utekelezaji wa mradi huo katika wilaya ya Chunya
Mkurugenzi mtendaji wa mradi huo pamoja na kujibu hoja toka kwa wadau amesema mapendekezo yanayowezekana kutekelezeka kwa sasa yatazingatiwa na kufanyiwa kazi huku akisisitiza ushiriki wa wadau hao kuhakikisha mradi huo unafanikiwa
Mradi huo unataraji kugharimu dola 79,159.18 ambayo ni zaidi ya milioni 180 na unataraji kuanza kutekelezwa Mapema mwezi june na kumalizika Mwezi desemba ambapo ni karibu miezi sita. Mradi huo unatekelezwa katika Mikoa Miwili yaani Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Mwanza ambapo kata kumi na Mbili zikihusishwa, Kwa Mkoa wa Mbeya Kata zote sita zinapatika wilayani Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.