Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mayeka Simon Mayeka amewataka Watendaji na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutekeleza majukumu ya usimamizi wa usafi na mazingira.
Mhe. Mayeka ameitoa rai hiyo leo alipohudhuria semina ya Mafunzo ya Utekelezaji wa Usafi wa mazingira iliyoendeshwa na AMREF kwa Watendaji wa Kata, Vijiji na Wataalam wa Halmashauri katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Mh. Mayeka alisema, suala la Usafi wa Mazingira ni jukumu la Serikali na kueleza kuwa, kama kuna washirika wanaosaidia jukumu hilo ni kwa sababu tu wameamua kusaidia.
“Usafi wa Mazingira ni suala la msingi la kwako, kama kuna taasisi au Shirika limekuja ni kutusaidia tu, mimi nilikuwa sioni kama ilikuwa sahihi AMREF waje kuhimiza ujenzi wa vyoo wakati kuna Mtendaji wa Kata, Kijiji na Afisa Tarafa”. Mh Mayeka alisema.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa, suala la ujenzi wa vyoo na usafi wa mazingira sio kazi ya AMREF bali ni kazi ya Serikali kuwahimiza wananchi kuwa na vyoo bora pamoja na usafi wa mazingira kiujulma.
"Niwashukuru sana AMREF kwa sababu hayo ni majukumu yetu, wanatusaidia lakini na sisi tunapaswa tuyachukue kama ya kwetu, tusiwaachie AMREF, isionekane ni majukumu yao." Alisema Mayeka.
"Kwenye Wilaya yetu suala la usafi wa mazingira kiukweli ni mbaya hali sio nzuri sana, mazingira yetu bado ni machafu hasa kwenye minada huko.
Aidha,Mhe. Mayeka amewataka viongozi hao kubadilika na kuanza kutimiza majukumu yao kiweledi kabla ya kusubiri msaada kutoka kwenye makampuni,mashirika au taasisi binafsi
“Mimi niwatake sasa baada ya mazungumzo ya leo mbadilike, nendeni mkafanye majukumu yenu, wala hakuna sababu ya kusubiria AMREF au mtu mwingine, hayo yapo ndani ya uwezo wenu, wewe upo Bitimanyanga mnada umeisha suala la usafi ni jukumu lenu kuhakikisha mnaacha mazingira yakiwa safi." Alisisitiza DC Mayeka.
Nae Mh. Alex Kinyamagoha Diwani wa Kata ya Itewe amesema, suala la usafi wa mazingiza kwa Wilaya ya Chunya bado lipo nyuma sana na mazingira mengi ni machafu.
“Binafsi nilipata bahati ya kutembea huko hasa tarafa ya kipembawe, hali ni mbaya, Chunya bado tuna kaya ambazo hazina vyoo.” Alisema Mhe. Kinyamagoha
"Wenzetu hawa wa AMREF wamekuja na suluhisho kwa wale wasioweza na wameshindwa kabisa, hawana vyanzo vya mapato, wamefanya muunganiko na watu wa Equit bank, wewe kama hauna fedha utakopeshwa na benki wao watakusimamia ufanye maendeleo, ujenge choo bora ili uepukane na maradhi ya mlipuko." Alisema Mhe. Kinyamagoha.
Watendaji wa Kata, Vijiji na Maafisa Elimu kata wakiwa katika Semina ya Mafunzo ya Utekelezaji wa Usafi na Mazingira iliyo endeshwa na AMREF kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Mayeka Simon MAyeka Akizungumza na Washiriki walioudhuria Mafunzo ya Utekelezaji wa Usafi wa Mazingira wilaya ya Chunya iliyoendeshwa na AMREF
Afisa Afya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bw. David Mwakasege Akiwasilisha mada kwenye Semina ya Utekelezaji wa Usafi wa Mazingira kwa Watendaji wa Kata,Vijiji pamoja na Maafisa Elimu kata waliohudhuria Semina hiyo iliyo ratibiwa na AMREF
Afisa Mradi wa AMREF Bi. Rebeca Magurusa Akielekeza jinsi ya Ujazwaji wa fomu mbalimbali za Majuimuisho ya Takwimu za Usafi wa Mazingira Ngazi ya Kata katika Kijiji kwa Watendaji wa Kata, Vijiji na Maofisa Elimu kata walio hudhuria Semina hiyo.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.