Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeendelea kung’ara katika mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jijini Dodoma kwa timu mbalimbali za watumishi kutoka Halmashauri zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku sababu kubwa ikitajwa kuwa namna Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuwa chachu kubwa ya Timu hiyo na hatimaye kesho kutupa karata yake dhidi ya Tanga Jiji kwa hatua ya kumi na sita bora
Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa upande wa mpira wa Miguu imeingia hatua ya kumi na sita bora baada ya kushinda michezo miwili, kudroo mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya wenyeji walima zabibu Dodoma Jiji hivyo kujikusanyika pointi saba nyuma ya Dodoma Jiji mwenye pointi 8, wakati huo huo timu ya mpira wa mikono (Handball bado iko hatua za makundi pamoja na Mpira wa pete (Netball) huku mchezo wa Riadha utaanza kesho
Akizungumza kwa njia ya simu kiongozi wa Msafara wa watumishi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambaye pia ndiye kocha wa timu ya mpira wa miguu Bwana Vicent Msolla amesema siri ya watumishi kujituma na kupambana ni kurudisha fadhira kwa Mkurugenzi jinsi anavyoishi na watumishi na hata kuridhia watumishi 35 kusafriri kwenda Dodoma kushiriki mashindano hayo kwani Halmashauri nyingine zimeshindwa na hata waliofanikiwa sio kwa idadi kubwa kama ilivyo Halmashauri ya wilaya ya Chunya
“Namna mwajiri anavyojitoa kwa watumishi, amekuwa ni chachu kubwa kwa hawa watu maana njia nzima wamekuwa wakimsema yeye tu na hata kuruhusu idadi kubwa ya watumishi kushiriki mashindano hayo maana ziko halmashauri zimeleta watu wawili au watatu
Pili mimi kama kiongozi wao nimewambia tunalo deni kubwa kwa halmashauri yetu hivyo lazima tuongeze bidii kuhakikisha tunafikia hatua ambayo ni nzuri
Kwaajili ya maandalizi ya hatua ya kumi na sita bora ambayo ni mtoano sisi tumekubaliana kwa pamoja kujitunza maana siri ya michezo ni kujitunza ili tufanye vizuri hatua ya kumi na sita bora maana timu zilizoingia ni bora kuliko hatua tulizovuka” Amesem Msolla
Naye Kapteni wa timu ya mpira wa Miguu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bwana Mshigati amesema siri ya Mafanikio ni uongozi bora wenye kuwapenda watu anaouonesha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya hivyo wachezaji wanaona hili ni deni la kulilipa kwa Halmashauri ya wilaya ya Chunya na namna pekee ya kulipa deni hilo ni kufanya vizuri kila hatua
“Kimsingi michezo hii ni ya watumishi hivyo sisi kama watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya tumejitoa kuipambania Halmashauri yetu, Wachezaji wana morali, kila mmoja anajitoa kwa jihadi kubwa na hatimaye tumevuka hatua ya makundi sasa tunaingia hatua ya mtoano.
Sababu kubwa kuliko zote ya sisi kufanya vizuri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya maana kitendo cha Kuruhusu wachezaji na viongozi 35 kuja kushiriki michezo hii sio kitu kidogo maana naweza kusema Chunya inaweza kuwa Halmashauri ya kwanza kuja na wachezaji wengi lakini pia tumetoka na gari yetu kutoka Chunya, na gari hiyo tunayo hapa Dodoma inatuchukua maeneo ambayo tunakaa kutupeleka viwanjani na kuturudisha jambo ambalo hauwezi kuliona kwa halmashauri zingine kwa hivyo hilo kwetu ni deni ambalo tunahangaika kulilipa kwa kiongozi wetu” Alisema Mshigati Kempteni wa timu ya mpira wa Miguu
Naye kepteni wa timu ya kuvuta kamba kwa upande wa wanawake Bi Devotha Mwasaga amesema wao kama Mabingwa watetezi bado timu kutoka Chunya ina khali ya kuchukua Ubingwa tena, huku akisikitika Kukosa wachumba wakati wa Mashindano hayo kutokana na namna ambavyo wamewabuluza wapinzani katika mashindano ya Vuta kamba
“Sisi huku kila tukipita tunaambiwa watumishi wanawake kutoka Chunya tunaogopwa na sababu ni mchezo wa kuvuta kamba na sababu iko wazi kabisa tumekuja tukiwa na maokoto ya kututosha na katika hilo lazima tumshukuru kiongozi wetu kutuwezesha kwa kiwango kikubwa namna hii” alisema Bi Mwasaga
Adha Bi Mwasaga amesema upande wa mpira wa pete (Netball) timu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imetolewa kwenye michuano huku sababu zikitajwa zikiwemo Mamluki kwenye timu nyingi za Halmashauri jambo ambalo Halmashauri mojawapo kuondolewa kwenye Mashindo kwa kutumia Mamluki wengi (kuchukua watu wasio watumishi), pia timu yao kutokujua kanuni mpya za mpira huo imepelekea kuwa na makosa mengi sana wakati wa michezo yao jambo lililo gharimu timu ya halmashauri ya wilaya ya Chunya
Pia Bi Mwasaga amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa namna alivyowawezesha kushiriki mashindano hayo pamoja na ushirikiano anaoendelea kuwapatia kwa kuwapo moya wakati wote na kwa kila hatua
Mashindano hayo yanahusisha michezo Mbalimbali kwa watumishi kutoka Halmashauri Mbalimbali huku Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikishiriki michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, handball, kuvuta kamba, karata na mchezo wa bao
Badhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakijianda kwa mazoezi kwenye moja ya viwanja vinavyotumika kwa mashindano ya SHIMISEMITA jijini Dodoma
Timu ya kuvuta Kamba ikiongoza na kampeni Devota Mwasaga (Kusho kwa aliyevaa kofia) wakiwa kwenye picha ya pamoja
Timu ya Mpira wa Pete ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye moja ya viwanja vinavyotumika kwa mashindano
Timu ya mpira wa miguu ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikiongozwa na Kocha Vicent Msola kushota kabla ya moja ya michezo yao hapo Jijini Dodoma
Timu ya mpira wa Miguu kabla ya Mchezo wao wakiwa wameshika Bendera ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuashiria wanaednelea kuiwakilisha vyema Halmashauri kwenye Mashindano hayo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.