Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauru ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim H. Kambona ametaka shirika la Hellen Keller Internation na shirika la Himalayan Cataract Project (HCP) na wadau kuendelea kuendelea kuja Chunya ili kuwahudumia wananchi wa wilaya yay a Chunya jambo ambalo litaendelea kuimarisha afya za wananchi wa Chunya na hata wananchi kutoka nje ya wilaya ya Chunya kwakufanya hivyo uchumi wa wananchi wa Chunya na Tanzania kwa ujumla utaendelea kuongezeka
Ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 24/6/2024 wakati alipowatembelea wanufaika wa huduma ya Uchunguzi na upasuaji wa Mtoto wa Jicho, pamoja na Madaktari bingwa wa Macho wanaoendelea kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa Macho (Mtoto wa Jicho) katika Hospitali ya wilaya ya Chunya, huduma iliyodumu kuanzia tarehe 19/6/2024 mpaka tarehe 24/06/2026
“Hili jambo linalofanyika kwa wilaya ya Chunya halijawahi fanyika hapo awali na limejumuisha wananchi wengi wenye matatizo ya macho wilayani Chunya na Nje ya wilaya ya Chunya huku wengine wakisafirishwa kwa zaidi ya kilometa 200 na wameendelea kupata matibabu. Lakini tumeshuhudia watu walikuwa hawawezi kuona kwa zaidi ya miaka mitatu, minne na wengine saba lakini sasa wanaona. Na wengine wameshuhudia hapa kwamba wamehangaika maeneo mengi bila mafanikio lakini kupitia hiki kinachofanyika hapa watu wamepata suluhu”.
Aidha Ndugu Kambona amewashukuru shirika la Hellen Keller Internation na shirika la Himalayan Cataract Project (HCP) kuendelea kutoa uelewa na ufahamu zaidi kwa watalamu wetu wa ndani kwani nao walikuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine ili kujipatia uzoefu na hatimaye hata zoezi hili litakapokuwa limehimitishwa basi wananchi wetu wataendelea kupata matibabu kupitia utaalamu na uzoefu walioupata lakini Hellen Keller Internation na shirika la Himalayan Cataract Project (HCP) watakapopata nafasi tena tunawakaribishwa kuja tena Chunya kutoa huduma kama hizi, Kwa niaba ya wananchi wote wa Chunya Tunawashukuru sana
Meneja wa mradi wa matibabu ya Macho Ndugu Athuman Tawaqal ametoa wito kwa mashirika mengine kuendelea kushirikiana na Serikali ili kutatua changamoto za wananchi wa Tanzania jambo ambalo litasaidia kuleta furaha kwa wananchi ambao wamekuwa na changamoto nyingi lakini wameshindwa kujipatia suluhu wao wenyewe na ameongeza kuwa changamoto ni kubwa sana hivyo nguvu Zaidi inatakiwa.
Kiongozi wa Jopo la Madaktari Bingwa Daktari Barnabas Mshangila anasema lengo lilikuwa kuwahudumia wananchi 450 wenye matatizo ya macho (Mtoto wa Jicho) lakini mpaka muda huu ikiwa ni siku ya mwisho tumesha hudumia wagongwa mia nne na ishirini hivyo ni matumaini yao lengo litafikiwa. Dkt Mshangila ameongeza kuwa huduma hii huleta furaha kwa watu wengi hasa pale ambapo mgonjwa alikuwa hajawai kuona na sasa kupitia huduma zilizotolewa zimemsaidia kuona tena hivyo lengo la kuleta matibabu linakuwa limefikiwa vizuri na limerudisha furaha kwa wananchi wa wilaya ya Chunya na hata watanzania kwa ujumla wake
“Tulimopokea binti mwenye mume na watoto wawili lakini kutokana na changamoto hiyo alikuwa hajawahi kuwaona watoto wake na hata mkewa hivyo kupitia huduma hii ameweza kuwaona watoto wake pamoja na mumewe hivyo alipata furaha” amesema Dakrati Mshangila
kKmbi ya Matibabu ya Macho ilianza rasmi tarehe 19/06/2024 na inataraji kuhimishwa tarehe 24/06/2024 huku mpaka saa nne asubuhi ya tarehe 24/06/2024 wagonjwa 420 walikuwa tayari wamepatiwa huduma. Huduma za uchunguzi na upasuaji zimetolewa bure kabisaa bila kujali umri, umbali na vigezo vingine vyovyote.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona (Aliyavaa suti) akiongozwa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya akiwasalimu wananchi wakiwa kwenye foleni ya kupatiwa huduma mapema leo
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya akifurahia jambo na Madaktari bingwa waliofika kwenye kambi ya matibabu ya Macho wakati alipowatembelea mapema leo
Kiongozi wa Jopo la Madaktari Bingwa Daktari Barnabas Mshangila akifafanua jambo wakati alipozungumza na waandishi wa Habari mapema leo katika viwanja vya hospitali ya wilaya ya Chunya
Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya Daktari Darison Andrew (Aliyenyoosha Mkono) akifafanua jambo wakati Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Chunya alipotembelea kambi ya matibabu ya Macho mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.