Afisa Mwandikishaji jimbo la Uchaguzi Lupa wakili Athuman Bamba ametoa wito kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi za kata kuzingatia yale yote watakayofundishwa ili yakawasaidie kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kwa weledi mkubwa katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura .
Wito huo umetolewa leo Desemba 19 /12/2024 wakati ufunguzi wa Mafunzo kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Ni muhimi mkazingatia yote mtakayofundishwa hapa, kwani Tume inatarajia baada ya mafunzo haya mtapaswa kutoa mafunzo haya kwa waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki na Waandishi wasaidizi ambao watahusika na Uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la kudumu la mpiga kura Vituoni “amesema Wakili Bamba
Sambamaba na wito huo, amewataka waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wenye uzoefu kuwasaidia waandikishaji wasaidizi wenzenu ambao hawajawahi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la mpiga kura ili waweze kutekeleza majukum yao kikamilifu na kwa weledi
Aidha amewataka Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kuvitunza vifaa vyote vya Uchaguzi vitakavyotumika katikia Uboreshaji wa daftari la mpiga kura ikiwa ni pamoja na kuzigatia maelekezo yote yatakayo tolewa na Tume katika zoezi la Uandikishaji ili muweze kuyafanyia kazi kwa usahihi na ufanisi wakati wa zoezi litakapokuwa limeanza.
Mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na namna ya ujazaji wa fomu wa fomu mbalimbali zitakazotumika wakati wa uandikishaji ,namna ya kutumia mfumo wa kuandikisha wapigakura(voters registration system VRS pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya uandikishaji wa wapiga kura. Mafunzo haya yameenda sambamba na kuapishwa kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata .
Mafunzo kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata yanatolewa na Maafisa waandikishaji wa jimbo la Lupa kwa siku mbili tarehe 19 na Tarehe 20/12/2024 ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa dafteri la kudumu la mpiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025 , Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Maafisa mbalimbali kutoka Tume ya Uchaguzi , Maafisa waandikishaji ngazi ya jimbo , Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Chunya, Afisa Uchaguzi Wilaya ya Chunya na Maafisa waandikishaji wasaidizi gazi ya Kata.
Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa wakili Athumani Bamba akifungua Mafunzo kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Jengo jipya la Utawala.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Chunya Mhe.James Mhanusi akitoa maelekezo kwa Maafisa waandikishaji wasaidizi kabla ya kuwaapisha Maafisa Hao wakati wa afunzo ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura .
Maafisa waandikishaji wasaidizi wakifuatilia somo la namna ya ujazaji wa fomu mbalimbali za uandikishaji wa wapigakura yaliyofundishwa na Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Lupa dkt Lukas Theodory katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri uliopo Jengo jipya la Utawala.
Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wakila kiapo wakati wa Mafunzo ya uboreshaji Daftari la kudumu la Mpiga kura yaliyotolewa katika ukumbi wa Halmashauri Jengi jipya la Utawala
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.