Ndugu Vincent Mbua kwa niaba ya Katibu tawala Mkoa wa Mbeya amewataka washiriki wa Mafunzo ya mfumo mpya wa ununuzi wa Umma kwa njia ya mtandao (NeST) kuwa chachu katika kutumia mfumo huo ili kuleta tija na ufanisi kwa serikari na jamii nzima kama serikali imekusudia .
Kauli hiyo imetolewa Jana Agosti 27, 2023 wakati wa akifunga Mafunzo ya mfumo mpya wa ununuzi wa Umma kwa njia ya mtandao (NeST) yaliyofanyika katiki ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya yaliyojumuisha Halmashauri zote saba (7) za Mkoa wa Mbeya
“Ninyi wote mlioshiriki mafunzo haya Kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya hakikisheni mnakuwa Chachu ya kuwaelewesha na kuwasaidia wale wanaopaswa kutumia huu mfumo wa NeST lakini pia kuhakikisha mfumo huu unaeleweka kule manakoenda na kuutekeleza kwa kuufanyia kazi kwa vitendo ili uweze kuwa ni mfumo wenye tija kama ulivyokusudiwa” alisema Mbua
Ndugu Mbua aliongeza kuwa Mafunzo mliyoyapata yakawasaidie ninyi katika kupunguza hoja za wakaguzi wa ndani na nje lakini pia kuongeza tija, uwazi na uwajibikaji kwa serikari kama ambavyo mfumo umelenge, pia mkaongeze ufanisi katika mifumo ya manunuzi kwa utendaji wenu mzuri kama Serikali ilivyo kusudia
“Ni matumaini yangu kuona hoja za ukaguzi katika mfumo huu wa ununuzi zinapungua kuputia mfumo huu mpya wa Ununuzi mliyoyapata kwa kuongeza umakini katika utendaji kazi wenu na kushirikiana vizuri na wakaguzi wenu wa ndani ili kuhakikisha Mfumo huu unakuwa na tija katika Halmashauri zetu” alisema Mbua
Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo ndugu Peter Tengu kutoka Busokelo amesema kuwa kupitia Mafunzo hayo ya mfumo mpya wa ununuzi unaolenga kupunguza mianya ya rushwa, kuongeza Uwazi na Uwajibikaji yatasaidia kuongeza ufanisi, kuboresha utendaji kazi na kuleta tija katika serikari na jamii kwa ujumla
Mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku 5 kuanzia tarehe 23/08/2023 na kuhitimishwa tarehe 27/08/2023 yamejumuisha Halmashauri zote saba za Mkoa wa Mbeya ambazo ni Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Rungwe, Busokelo, Mbyeya jiji na Mbeya vjijini, Mbalali na Kyela yamehusisha Maafisa Manunuzi, Wakaguzi wa ndani, Maafisa Tehama, Wanasheria , Maafisa habari na Maafisa Mipango.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.