Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa wakili Athuman Bamba amewataka Waandikishaji wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki kuhakikisha wanatumia weledi na ubora uliowapa nafasi ya kuteuliwa na tume kutekeleza jukumu la uboreshaji wa daftari la mpiga kura huku akiwahimiza kutumia vizuri na kuvitunza vifaa watakavyokabidhiwa kwaajili ya kazi.
Hayo ameyasema leo tarehe 23/12/2024 wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wasaidizi wa vituo na waendesha vifaa vya Bayometriki yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo)
“Ninatoa wito kwenu kuhakikisha mnatumia vizuri vifaa hivyo ,mnavitunza vifaa vyote vitakavyotumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura kwa kuzingatia maelekezo yatakayotolewa na tume kwani kwa kufanya hivyo mtafanya kazi kwa usahihi na kwa weledi wakati wa zoezi litakapokuwa limeanza”amesema Wakili Bamba.
Aidha wakili Bamba amewasisitiza waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki kuzingatia mafunzo yote yatakayofundishwa ili wakafanye kazi inayotarajiwa kwa weledi ,bidii moyo na kujituma pamoja na kutumia uzoefu wao kuwasaidia wenzao ambao hawana uzoefu ili zoezi liweze kufanyika kwa usahihi na weledi mkubwa
Mafunzo yameenda sambamba na kuapishwa kwa Waandikishaji wasaidizi na waendesha Vifaa vya bayometriki pamoja na kufundishwa mada mbalimbali juu ya namna bora ya ujazaji wa fomu mbalimbali zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura, kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (voters registration system VRS) pamoja na matumizi sahihi ya ya vifaa vya uandikishaji wa wapiga kura .
Mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki jimbo la Lupa yanatolewa na Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kwa kusaidiana na Maafisa wa Tume kutoka Halmashauri na Makao makuu, Mafunzo hayo yatadumu kwa siku mbili tarehe 23/12 na Tarehe 24/12/2024 ikiwa ni maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura litakaloanza tarehe 27/12/2024 na kuhitimishwa Tarehe 02/01/2025 ikiwa ni maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka Octoba 2025.
“Kujiandikisha kwa Mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora”.
Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa Wakili Athuman Bamba akizungumza na waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki wakati akifungua mafunzo katika Ukumbi wa Sapanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Waandikishaji wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki wakiapa wakati wa Mafunzo ya Uboreshaji daftari lakudum la Mpiga kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sapanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Afisa Mwandikishaji Msaidizi ngazi ya kata ndugu Ntundu Chapa akifundisha namna ya ujazaji wa fomu mbalimbali wakati wa mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa jimbo la Lupa
Waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki wakifuatilia mafunzo yanayoendelea kutolewa na Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata katika Ukumbi wa Sapanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.