KATIBU Tawala wilaya ya Chunya Bw. Anaklet Michombero amewataka Watendaji wa kata na vijiji wilayani chunya kuhakikisha shule zote ndani ya wilaya zinatoa chakula na lishe kwa wanafunzi wakiwa shule kwani ni suala muhimu
Michombero ameyasema hayo jana tarehe 31 January 2023 wakati akiongoza kikao cha kamati ya lishe cha robo ya pili ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri (Sapanjo) ambapo amesema wanafunzi wanapokosa chakula shuleni hukosa usikivu mzuri wakati wa ujifunzaji.
Aliongeza kuwa katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama mkoa (RCC) walikubaliana kwa pamoja kwamba kila shule lazima itoe chakula na lishe kwa wanafunzi, hivyo watendaji na maafisa elimu kata hakikisheni mnasimamia maagizo hayo .
Akiwasilisha taarifa ya lishe kaimu afisa lishe wilaya ya chunya Bi. Mariam Thomas amesema wanaendelea na juhudi za kuhakikisha lishe inapatikana katika shule zote za wilaya ya chunya
Aidha amesema kitengo cha lishe kimefanikiwa kuwafikia watoto 39,243 sawa na asilimia 90 kati ya lengo la kuwafikia watoto 43,679, vilevile amesema watoto 23,713 sawa na asilimia 60.4% walikutwa na hali nzuri ya lishe na watoto 10,989 sawa na asilimia 28% walikutwa na hali ya udumavu huku watoto 4,512 sawa na asilimia 11.5%walikutwa na utapiamlo.
Wajumbe wa kamati ya lishe wilaya ya chunya wakiwa katika kikao cha lishe cha robo ya pili kwa mwaka 2022/2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.