KATIBU Tawala wa Wilaya ya Chunya Mh Anaklet Michombero amewaongoza wakazi wa Wilaya ya Chunya na viongozi mbalimbali kufanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Wilaya, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Michombero alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kuhakikisha wanashiriki zoezi la sensa pindi ifikapo Agosti 23, 20222.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndg. Tamim Kambona amesema wao kama halmashauri wameamua kuadhimisha muungano kwa kusafisha mazingira ya hospitali ya Wilaya.
“Kama maagizo ya Serikali yalivyotolewa siku hii ya leo itahadhimishwa kwa wananchi kufanya usafi katika eneo mojawapo la taasisi ambalo litakuwa limechaguliwa kwa ajili ya kufanya usafi huo.
“Na kwa Halmashauri ya Wilaya yetu ya Chunya tulikubaliana usafi ufanyike kwenye eneo letu la hospitali.” Alisema Kambona
Pia Kambona aliwapongeza na kuwashukuru wananchi kwa namna walivyojitoa na kushiriki usafi katika hospitali ya Wilaya na kuhakikisha mazingira ya hospitali yanakuwa safi.
Aidha Katibu wa CCM Wilaya ya Chunya Mh. Charles J. Seleman akizungumza baada ya zoezi la usafi kumalizika amesema, moja ya mafanikio ya muungano ni maendeleo yaliyopo Wilayani Chunya.
“Maendeleo tunayoyaona katika wilaya yetu yapo wazi ambayo wewe kama mkuu wa Serikali na Mkurugenzi mmeyasimamia na yameletea tija katika wilaya yetu.” Alisema Seleman.
Waki huo huo, Katibu huyo amewasisitiza wanachunya kuendelea kuwa na umoja, upendo na mshikamano ili kuweza kuiletea Chunya maendeleo.
“Ndugu zangu wananchunya kinachotakiwa sasa ni kujenga ushirikiano wa pamoja, umoja, upendo na mshikamano katika kuleta mandeleo ya Wilaya yetu ya Chunya”. Alisema Seleman.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndg Tamim Kambona Akifweka Majani Katika Eneo la Hospitali ya Wilaya ikiwa Ni Maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Chunya waliojitokeza na kushiriki kufanya Usafi katika Eneo la Hospitali ya Wilaya, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg John Maholani wa kwanza kushoto akiwa sambamba na moja wa mwananchi aliyejitokeza kufanya usafi katika hospitali ya wilaya
Mr. Joel Joel Afisa Hesabu II Halmashauri ya wilaya ya Chunya Akifanya Usafi katika Moja ya Eneo la hopsitali ya Wilaya, Ikiwa Maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.