Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe.Bosco Mwanginde amewataka maafisa Maendeleo wa Kata waliokabidhiwa vipaza sauti kwaajili ya kuwarahisishia utendaji kazi wao na kuweza kuwafikia na kuwahudumia wananchi wengi kuhakikisha wanavitumia vipaza sauti hivyo kwa shughuli iliyokusudiwa na kwa matumizi mengine ili kutimiza adhima ya serikali ya kuwafikia Wananchi na kuwahudumia katika maeneo yao.
Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 15, 2024 katika jengo la Halmashauri wakati akikabidhi vipaza sauti 9 vilivyogharimu kiasi cha shilingi million nne na laki tisa (Tsh. 4,950,000/=) kwa maafisa maendeleo ya jamii wa kata.
“Naomba sana tukavitumie vipaza sauti hivi katika shughuli ambazo zitanufaisha kata husika na sivinginevyo kama tutaona vinatumika tofauti kama kwenye harusi na shughuli nyingine hatutasita kuchukua hatua dhidi ya afisa huyo , vyombo hivi vinatakiwa vikatunzwe vizuri ili viweze kutumika kwa muda mrefu”Amesema Mhe. Mwanginde.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ndugu Tamim Kambona amesema kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa ikiwa ni maagizo ya serikali kuhakikisha kila Halmashauri inawanunulia vipaza sauti Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata kwaajili ya shughuli za uhamasishaji na utoaji wa elimu kuhusu mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani.
Kaimu Afisa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bi Ester Kondobole amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imetekeleza agizo la Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia wanawake na Makundi maalumu kwa kununua vipaza sauti kwa lengo la kufanya kazi za uhamasishaji jamii kwa suala la maendeleo , mikopo na miradi ya maendeleo pamoja na mambo mengine yenye tija katika jamii.
Erick Msola,Twijisye Ephraim, Kaiza Sanga na Noelia Mwambela wakiwawakilisha Maafisa Maendeleo wenzao ngazi ya kata wameishukuru serikali kwa kuwanunulia vipaza suti kwani vitawasaidia kuwafikia wananchi wengi katika kutoa elimu kuhusu mikopo inayotolewa na Halmashauri, elimu ya ukatili wa kijinsia na masuala ya maendeleo katika jamii kwenye maeneo mbalimbali kama vile magulioni, Shuleni na Mikutano ya Hadhara na maeneo mengine.
Vipaza sauti hivyo 9 vimetolewa kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata katika kata 9 za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambazo ni kata ya Sangambi, Chalangwa, Chokaa, Mamba, Makongolosi, Mbugani, mkola , Lualaje na Matundasi ikiwa ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo na kwa awamu ya pili vipaza sauti vitagaiwa kwenye kata zilizosalia.
Mwnyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde akimkabidhi kipaza sauti Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Sangambi ndugu Erick Msola katika Jengo la Halmashauri .
Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Wilaya na Kata kwenye picha ya pamoja wakati wa kukabidhiwa vipaza sauti kwa Maafisa Maendeleo ngazi ya Kata katika Jengo la Halmashauri .
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.