Mkuu wa wilaya ya Chunya mhe.Mbaraka Alhaji Batenga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka wananchi kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari, kwani Ugonjwa wa Ukimwi bado upo licha ya juhudi ambazo zinaendelea kufanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, bado tiba na chanjo ya ugonjwa huo bado haijapatikana.
Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 1/ 2024 katika siku ya Maadhimisho ya UKIMWI duniani yamefanyika kimkoa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Itete kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya yaliyobebe kauli mbiu isemayo “Chagua njia sahihi, tokomeza UKIMWI" ambapo jamii imeweza kuchangia damu kupima pressure na kisukari pamoja na kupata elimu.
“Niwaombe ndugu zangu tuendelee kujitokeza kupima afya zetu kwani UKIMWI bado upo pamoja na jitihada ambazo zinaendelea kufanyika lakini Tiba bado haijapatikana wala chanjo bado haijapatikana tukilitambua hilo tutaendelea kujikumbusha kwamba UKIMWI bado upo hivyo tuishi kwa kujikinga na kuchukua tahadhari “amesema Mhe. Batenga.
Aidha Mhe Batenga ameongeza kuwa msingi wa kwanza wa mtu ni kuwa na afya njema kwani maendeleo pesa na mambo mengine yanapatikana kwa kuwa na Afya njema huku akitoa rai kwa wanaume kujitokeza kupima Afya zao badala ya kutegemea vipimo vya wake zao kwamba majibu ya wake zao ndio majibu yao kwani jambo hilo si sahihi afya ni jambo la mtu binafsi na si jambo la familia.
“Wanaume achene kutembea na majibu ya vipimo vya wake zenu hasa yanapokuja majibu mazuri,Wanaume acheni tabia hiyo kwani anayepata ugonjwa huu ni mtu na si familia na si lazima mke akiugua na mume naye lazima augue au mke akiwa mzima na mume lazima awe mzima hivyo kila mtu akapime yeye mwenyewe ajue afya yake na si kuulizia majibu ya mtu mwingine” amesema Mhe.Batenga
Awali akitoa salam katika Maadhimisho diwani wa kata ya Ifumbo Mhe Weston Mpyila kwaniaba ya wanachunya na wananchi wa Ifimbo ameshukuru maadhimisho hayo kuadhimishwa katika Wilaya ya Chunya kimkoa kwani imekuwa nafasi nzuri ya wao kujifunza kupitia mada mbalimbali kutoka kwa Wadau na wataalam lakini pia nyimbo na burudani zenye jumbe tofauti tofauti ili kutoa elimu kuhusu Ugonjwa wa UKIMWI ili jamii iendelee kuchukua tahadhari na kuendelea kujikinga
Akisoma taarifa ya hali ya utowaji wa huduma za VVU na UKIMWI Mratibu huduma za Ukimwi Mkoa wa Mbeya Dkt Deo Magongwe amesema kuwa lengo la maadhimisho ni kuongeza uelewa katika jamii na kuijulisha jamii kufahamu mafanikio na changamoto zinazoikabili dunia juu ya tatizo la maambukizi ya VVU na UKIMWI pamoja na kuandaa mikakati mbalimbali ya namna ya kukabiliananazo
Wadau mbalimbali wakiwemo SHDEFHA, DSW ,NIMRI kwa pamoja wameendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na kuendelea kuchukua tahadari dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ikiwa ni pamoja na kuhamasisha jamii kuendelea kupima Afya zao, kutumia kinga ili kulinda Afya zao kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla .
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani huadhimishwa kila mwaka Tarehe 1 Desemba ili kuelimisha jamii dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kuchukua tahadhari, katika Mkoa wa Mbeya Maadhimisho haya yamefanyika Wilaya ya Chunya ambapo yamehudhuriwa na watalamu mbalimbali kutoa Mkoani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Vikundi vya burudani na Wananchi.
Mkuu wa Wilayaya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga ametembelea banda la damu salama kujionea wananchi wakichangia damu wakati wa Maadhimisho ya siku ya UKIMWI dunani iliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Chunya.
Diwani wa kata ya Ifumbo Me.Weston Mpyila akieleza namna ambavyo elimu waliyoipata itawasaidia kuendelea kuchukua tahadhari na kujikinga dhidi ya UKIMWI wakati wa maadhimisho siku ya UKIMWI duniani yaliyoadhimishwa katika kata ya Ifumbo Uwanja wa Shule ya Msingi Itete.
Mratibu wa huduma za UKIMWI Mkoa wa Mbeya Dkt Deo Magongwe akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na UKIMWI Mkoa wa Mbeya wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI yaliyofanyika Wilayani Chunya.
Mkuu wa Wilayya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka shirika la DSWpamoja na wataalam mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani wilayani Chunya
Wananchi wa kata ya Ifumbo wakifuatilia elimu mbalimbali kuhusu UKIMWI wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Itete kata ya Ifumbo.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.