Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaji Batenga amewataka viongozi wapya wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa serikali za Vijiji kuwatendea haki wananchi waliowachagua kwa kutekeleza majukum yao , kusikiliza kero za wananchi na kutenda haki bila kujali nafasi aliyonayo mtu kwani wamechaguliwa ili kuwahudumia wananchi .
Kauli hiyo ametoa leo Desemba 8/2024 wakati wa mafunzo kwa viongozi na wajumbe wapya wa serikali za Vijiji , Vitongoji na Wajumbe yaliyofanyika katika Tarafa ya Kipembawe kata ya Lupa Ukumbi wa Shule ye Sekondari Lupa
“Serikali imetumia gharama kubwa sana kuwaweka ninyi madarakani kwasababu ninyi ndio ngazi ya kwanza kabisa ya utawala wa serikali na wananchi wa Nchi hii mnaishi nao ninyi , hivyo mkumbuke wananchi kuipenda serikali kunatokana na ninyi na kuichukia serikali kunatokana na ninyi kwahiyo mwende mkawatendee haki Wnananchi hawa tusiende kuichonganisha serikali na Wananchi” amesema Mhe .Batenga
Aidha Mhe Batenga ameendelea kutoa msisitizo kwa Viingozi wa serikali za Vijiji na Vitongoji kwenda kusimamia daftari la kitongiji la kuwasajili watu kuhakikisha kila kitongoji kinakuwa na daftari hai kwani daftari la kitongoji la kuwasajili watu si la kisiasa hiyo itasaidia kujua watu wanaoinga katika kijiji lakini pia itasidia hata katika mambo mengine ya kiusalama pamoja na ugawaji wa ardhi.
Akitoa salamu za Chama Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya ndugu Noel Chiwanga amewataka watendaji wa kata na vijiji wao kama watalaam kuwasaidia wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na si vinginevyo lakini pia ametoa rai kwa wenyeviti wa vijiji na Vitongoji kuto kutumika vibaya badala yake wakawasaidie na kuwahudumia Wananchi wao.
“Naninyi wenyeviti msiende kutumika vibaya, angalieni matatizo ya wananchi katika maeneo yenu husika na mkayatatue mkawaoneshe wananchi kwamba mko kwaajili yao, lakini pia Katika kila kijiji na kitongoji kuna miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na mama Samia nendeni mkaiseme hiyo kwa wanannchi lakini pia mkaisimimie vyema “ amesema Chiwanga
Naye kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Cuthbeth Mwinuka ametoa rai kwa viongozi wa serikali za mitaa kwenda kusimamia maeneo yao ikiwa ni pamoja na kufuata sheri na taratibu za ukataji wa miti kwaajili ya shughuli mbalimbali lakini pia kuyatunza mashamba yote ambayo yametengwa na serikali kwaajili ya kilimo pamoja na kusimamia na kuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi ambayo imewekwa.
Mafunzo kwa wenyeviti wa vijiji, vitongoji na Wajumbe wa serikali za Vijiji kwa tarafa ya Kipembawe yamefanyika leo tarehe 8 Desemba 2024 na yatahitimishwa kesho tarehe 9 Desemba 2024 kwa Tarafa ya Kiwanja ambapo mada mbalimbali zimefundishwa ikiwa ni pamoja na elimu ya Rushwa, Ulinzi na Usalama ,Majukumu ya wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, aina za ardhi , ukusanyaji wa mapato ,Utunzaji wa Mazingira , elimu kuhusu Mfumo wa manunizi na mada nyingine .
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akioongea na Viongozi wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa serikali za Vijiji juu ya kuwatumikia wananchi waliowachagua wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa viongozi hao katika Tarafa ya Kipembawe .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akitoa salam za Chama kwa Viongozi wa serikali za Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa serikali za Vijiji wakati wa Mafunzo kwa Viongozi hao Tarafa ya Kipembawe.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya Nestory Mwita akifundisha mada ua Ulinzi na Usalama kwa Viongozi wa serikali za Vijiji,Vitongoji na Wajumbe wa serikali za Vijiji
Mkuu wa kitengo cha Maliasili Dkt Theodory Lukasi akifundisha mada ya utunzaji wa Mazingira kwa wajumbe wa Serikali za Vijiji,Vitongoji na Wajumbe wa serikali za vijiji katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lupa
wENYEVITI WA VIJIJI,Vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wakufunzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lupa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.