Baraza la Madiwani kupitia Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewataka Mafundi wote wanaojenga Miundombinu Mbalimbali ya Elimu Na miundombinu mingine wilayani Chunya Kukamilisha kwa muda stahiki kama mikataba inavyoelekeza ili wanafunzi waanze kutumia miundombinu hiyo jambo litakalosaidia kurahisisha zoezi la Ufundishaji na Ujifunzaji na hatimaye kupata ufaulu mzuri
Akitoa maelekezo hayo kwa niaba ya kamati hiyo leo tarehe02/04/2024 Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Ramadhan Shumbi amewataka viongozi wa kijiji na kata wanaosimamia ujenzi wa Madarasa matatu na ofisi katika Shule ya Msingi Chunya Mjini kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo ndani ya Muda ili wanafunzi waanze kutumia madarasa hayo na hatimaye kufanya vizuri katika mitihani yao huku akiwakumbusha kwamba Halmashauri ya wilaya ya Chunya Haihitaji ufaulu mbaya.
“Hakikisheni mnamaliza ujenzi wa Miundombinu ya Elimu na miundombinu inayojengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa wakati, sisi hatutaki kufeli kwenye masomo hivyo mmalize mapema ujenzi huu kama mkataba unavyotaka ili watoto waanze kutumia miundombinu hii kama Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anavyotaka”Amesema Mhe Shumbi
Aidha Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya amewapongeza wananchi wa kijiji cha Chunya Mjini kwa namna wanavyoshiriki kwenye ujenzi wa mradi huo lakini kuamua kujitolea kujenga madarasa manne na ofisi kwa Nguvu zao, jambo ambalo Makamu Mwenyekiti amesema jamii ya wananchi wa Chunya wanapaswa kujifunza na kuiga
Kwa niaba ya viongozi na wananchi wa kata ya Itewe diwani wa kata hiyo Mhe Alex Kinyamagoha amewashukuru wajumbe wa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa namna ambavyo wameendelea kuwatazama wananchi wa Itewe kwa kuwapatia fedha za kujenga miradi mbalimbali ya Elimu
“Kwa niaba ya wananchi wa Itewe pamoja na viongozi wenzangu naomba nikushukuru wewe mwenyekiti pamoja na kamati yako na baraza kwa ujumla kwa namna mnavyojali wananchi wa kata ya Itewe maana mnawasikiliza na kutatua kero zao na ndio maana mmetuletea fedha nyingi za kujenga miradi mbalimbali ya Elimu Hapa Shule ya Msingi Chunya mjini lakini pia pale kwenye Sekondari yetu ya kata lakini pia nimshukuru Mkurugenzi mtendaji kwa kutupatia wahandisi mahiri wanaosimamia miradi nitambue kazi yao mbele yako kwamba ni nzuri na njema ila ombi langu ni moja tunaomba wapatiwe usafiri ili waweze kutembea maeneo mengi kwa wakati.” Amesema Kinyamagoha
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ipo katika ziara yake ya kawaida ikiwa katika siku yake ya kwanza imekagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shule ya msingi Makongolosi, Imekagua vifaa tiba kituo cha Afya Makongolosi, Imekagua ujenzi wa Chumba kimoja cha darasa na ujenzi wa matundu nane ya vyoo shule ya sekondari Makalla, Ujenzi wa Zahanati ya Sambilimwaya, Ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Chunya Mjini, Ukarabati wa madarasa kumi na moja Shule ya sekondari ya kata Itewe na kuhitimisha siku ya kwanza kwa kukagua ujenzi wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi Kibaoni ambapo miradi yote inagharimu shilingi milioni 598,400,000/=
Afisa Elimu awali na msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mwalim Ferd Y. Mhanze akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya mapema leo walipotembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Makongolosi
Mfamasia wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Edward Tengulaga akifafanua Jambo mbele ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya mapema leo ilipotembelea kukagua mapokezi ya Vifaa vya Shilingi Milioni mia mbili katika kituo cha Afya cha Makongolosi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.