Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde ametoa rai kwa waheshimiwa madiwani kuhakikisha miradi yote inayoanzishwa kwa nguvu za wananchi inakamilika kwa asilimia miamoja (100%) na sio kutegemea Halmashauri kukamilisha miradi hiyo , halmashauri itaongeza nguvu pale itakapo wezekana kufanya hivyo.
Kauli hiyo ameotoa Mhe. Mwanginde tarehe 27/01/2025 wakati wa kikao cha baraza la kujadili na kupitia randama ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri jengo jipya la utawala.
Miradi yote inayoanzishwa kule kwenye vijiji na kata ni miradi ya kwetu Madiwani kwa wananchi wetu, tunatakiwa kuianzisha miradi na kuikamilisha kwa asilimia mia moja(100%), pale tunapokuwa na uwezo katika Halmashauri basi Halmashauri itaongeza nguvu lakini sio kuanzisha mradi na kuachia njiani kwamba Halmashauri itamalizia kwani hiyo inaweza kusababisha mradi kuchukua muda mrefu kukamilika. Amesisitiza Mhe. Mwanginde.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga ametoa pongezi kwa vyama vya siasa na waheshimiwa madiwani kwa kufanikisha uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mafanikio makubwa, amani na utulivu nakusihi hali hiyo iendelee hadi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2025.
Aidha, Mhe.Baenga amewaeleza waheshimiwa madiwani kusudi la Halmashauri kuanzisha kituo cha redio cha Halmashauri kitakachosaidia kufikisha taarifa na elimu ya mambo mbalimbali kwa wananchi wa Chunya na maeneo jirani kwa uraisi zaidi, Vilevile, amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanyika katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ambapo hadi mwezi January 2025, Halmashauri imekusanya mapato Tsh. Bilioni 7.9 sawa na asilimia tisini na moja (91%) ya lengo la makadirio ya kukusanya Tsh. Billion 8.7 iliyopangwa kukusanywa kwa mwaka.
Afisa mipango na uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Janeth Mwaigoga akisoma randama ya mpango wa bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa mwaka wa fedha 2025/2026 amesema kuwa vipaumbele vya halmashauri katika bajeti hiyo ni pamoja na kutenga fedha na kuviwezesha vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, kuboresha huduma za kijamii, kuongeza ukusanyaji wa mapato pamoja na mambo mengine mengi.
Kikao cha baraza cha kujadili na kupitia makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani, kamati ya ulinzi na usalama, wataalamu wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya , wataalamu kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wadau wa vyama vya siasa.
Afisa mipango na uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bi Janeth Mwaigoga Akisoma randama ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 wakati wa kikao cha baraza cha kujadili randama hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akitoa pengezi kwa waheshimiwa madiwani na wajumbe wa kikao cha balaza la kujadili radama ya bajeti kwa mwaka 2025/2026 kilichoketi ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri jengo jiya la Utawala.
Diwani wa kata ya Lupa Mhe Daniel Mwafyele akitaka ufafanuzi juu ya miradi itakayotekelezwa wakati wa kikao cha kujadili randama ya bajetii kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.