Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka amewataka viongozi wa serikali ngazi ya vijiji na kata kuacha mara moja kuwakamata wananchi kwa kuwaonea jambo ambalo sio lengo la serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wake wakiwepo wananchi wa Chunya na Kata ya Ifumbo.
Ametoa Katazo hilo tarehe 11/10/2023 alipokuwa katika kijiji cha LupaMarket kilichopo kata ya Ifumbo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoianza mapema tarehe 2/10/2023 sambamba na hilo ameagiza kusomwa na kubandikwa hadharani taarifa za mapato na matumizi ya fedha kwa ngazi za vijiji ili wananchi waweze kujua fedha za serikali zinatumikaje pamoja na fedha wanazokuwa wamechangia wao wenyewe.
“Kukamata watu kwakuwaonea mkome mara moja, ila kama umefanya kosa ni haki yako kukamatwa na pia ni haki yako kupigwa faini. Ikitokea umekamatwa kwakuonewa nipe taarifa mimi nitachukua hatua mara moja maana sipendi wananchi wa jimbo la Lupa kuonewa Na pia kusoma na kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha za serikali na fedha walizochangia wananchi kwa lengo la maendeleo au lengo lingine lolote ni takwa la kisheria, kupitia mkutano huu nawaagiza watendaji wote wa serikali kuwasomea mapato na matumizi wananchi kutokufanya hivyo mnakiuka sheria na taratibu” Alisema Mhe Masache
Kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Jimbo la Lupa, Diwani wa kata ya Lupa Mhe. Weston S. Mpyila amesema kwa sasa changamoto ya wananchi wa kata ya Ifumbo ni ukamilishaji wa kituo cha Afya kinachojengwa kwenye kata hiyo kwani idadi ya wananchi wa kata hiyo imeongezeka sana jambo linalopelekea zahanati zilizopo kushindwa kuwahudumia ipasavyo, Pia Mhe Mpyila amekiri kupokea vitanda sita katia zahanati ya LupaMarket, kupokea fedha za ujenzi wa madarasa shule ya Msing LupaMarket pia ameishukuru serikali kuifungua barabara ya Kiwanja-Ifumbo ambapo zaidi ya shilingi milioni mia nne na hamsini zimetumika kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha changalawe.
“Tumepokea vitanda sita (6) zahanati ya Luapamerket, Jengo la wagonjwa wa nje limejengwa pale kwenye kituo cha Afya bado vitu vichache, pamoja na kuwa na zahanati mbili lakini kwasasa idadi ya wananchi wa Ifumbo imeongezeka hivyo uhitaji wa kituo cha Afya ni mkubwa sana”. Pia Mhe Diwani wakati anatoa salamu kwenye mkutano wa Mhe Mbunge kwenye kijiji cha Ifumbo ameseme “… wana Ifumbo kwasasa wamestaraabika hivyo hawahitaji kusukumwa sukumwa , na viongozi wa serikali ngazi ya kata na vijiji wapo hapa waendelee kutekeleza hilo”.
Kwa ruhusa ya Mhe Mbunge, akijibu kero ya wananchi ya kutozwa michango bila kupewa risiti pamoja na kutosomewa mapato na matumizi Afisa mipango wa wilaya ya Chunya kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Ndugu Mjanaheri Swalehe amesema ni kosa kutokusoma mapato na matumzi kwa wananchi na pia ni kosa kutokutoa risiti kwa mtu yeyote anapotoa pesa yoyote au michango mbalimbali ambayo ipi kisheria au mmekubaliana hivyo kupitia hadhara hiyo amewataka watumishi wote kwenye maeneo yao ya kazi wafuate taratibu za utumishi wa umma.
Mueda Muliemo, Michael Munis, Nichoraus Mwasinyanga na Faraja Mwasimba waliuliza maswali kwa niaba ya wananchi wengine kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Lupamarket wakati Brayson Daimon Mwasimba,Abeli Mlangali, Elia Wiston Waya na Veronica Mpilla waliwawakilisha wananchi wengine kuuliza maswali mbalimbali kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Ifumbo.
Changamoto kubwa iliyozungumzwa na wananchi wengi na kwa hisia kali ni uvamizi wa kampuni ya kichina kuchimba kwenye maeneo yaliyokazwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2018 wakati akiwa makamu wa Rais lakini pia Mkuu wa wilaya ya amekuwa akikemea mara kwa mara kupitia mikutano yake kwenye kata ya Ifumbo kuhusu kutokuchimba kwenye vyanzo vya maji ikiwepo kwenye mto Zilla lakini kwasasa wananchi wanashangazwa kupewa mtu mwingine ambaye si mwenyeji wa eneo hilo kuanza kufanya shughuli zile zile ambazo wao wamekatazwa.
Mhe Masache amewataka wananchi wa Ifumbo kuwa watulivu wakati yeye kama mwakilishi wao anafuta suluhu ya kero hiyo ambayo imeonekana ni kero kubwa na inawaumiza wananchi wa kata ya Ifumbo huku wananchi hao wakishindwa kuelewa ni serikali ipi imeruhusu maeneo ambayo wao walikatazwa na walitii makazo hayo kwa muda mrefu kuanza kuchimbwa na mtu mwingine ambaye siye mwenyeji.
Ziara ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa katika kata ya Ifumbo imehitimisha safari ya kutembelea kata zote 20 za jimbo la Lupa na kero mbalimbali zikipatiawa suluhu na nyingine ambazo zinahusisha mamlaka Mbali mabali ameahidi kuzishughulikia kwa wakati kulingana na uharaka wake lakini amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwani kila changamoto ya mwananchi inachukuliwa kwa uzito unaostahili
Diwani wa Kata ya Ifumbo Mh. Weston S. Mpyila akizungumza mbele ya wananchi wa Kijiji cha Ifumbo kabla ya Kumkaribisha Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasasa wakati alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wananchi wake
Afisa Mipango Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Mnajaheri Swalehe akijibu kero ya wananchi kutosomewa mapato na Matumizi pamoja na kutokua risiti mwananchi anapoa mchango au fedha zilizowekwa kisheria wakati wa mkutano wa Mbunge kwenye kijiji cha Lupamarket
Veronica Mpyilla mwananchi wa kijiji cha Ifumbo akiulizwa swali kwa Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa wakati alipofanya ziara ya kuzungmza na wananchi katika kijiji hicho
Mapokezi ya Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka kwenye kijiji cha LupaMarket wakati alipokuwa anawasili kwaajili ya Mkutano (Wananchi walitandika ngup zao kwa Umbali wa Zaidi ya Mita mia moja ili Mbunge apite juu ya Nguo mkapa eneo la Mkutano)
Wananchi wa Kijiji cha Ifumbo wakimsikiliza Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache wakati alipowatembelea kusikiliza kero za wananchi hao
Wananchi wa Ifumbo wakiendelea kumsikilza Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.