Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka amesema kazi yake iliyompeleka Bunge ni kuwasemea wananchi wa jimbo la Lupa hivyo amewataka wananchi kuendelea kumtuma kuwasemea kwani kazi hiyo bado ana imuda sawasawa huku akiwataka wananchi kurejelea yale mambo waliyomtuma awali mengine yameanza kutekelezwa na mengine mengi yamekamilika kwa asilimia kubwa sana
Mhe Masache ametoa kauli hiyo ijumaa tarehe 28/7/2023 alipokuwa anazungmzra na wananchi wa Kata ya Itwe ambapo alifanya Mkutano katika viwanja vya soko la Chunya Mjini na Baadaye amefanya Mkutano mwingine katika kijiji cha Sinjilili A huku azma yake ni kurudisha mrejesho kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayotekelezwa na serikali katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chunya ambayo awali ilikuwa ni kero kubwa wananchi wengi
“Nimekuja kuwapeni mrejesho wa kwanza Bunge la Bajeti lililokamilika hivi karibuni ili mjue nini kimepangwa na utekelezaji wake utakuwaje, lakini pia kuwambiaeni namna ambavyoserikali inatekeleza mradi mbalimbali katika maeneo yetu baada ya mimi mliyenituma kusema mnachokihitaji na mwisho kuomba mnitume tena bungeni kuendelea kuwasemea kwa mambo mengine yanayowakabiri na mnataka serikali itusaidie kuyatekeleza”
Mhe Masache ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo inatoa fedha nyingi ili kutekeleza miradi mbalimbali wilayani Chunya huku akisema wananchi wao ni mashahidi kwani miradi mbalimbali imetekelez2wa katika amaeneo yao huku akirejea ujenzi wa Taa za Barabarani, Chunya, mjini, Matundasu na Makongosi, Miradi ya maji inayotekelezwa ambayo italeta suluhu ya Changamoto ya maji wilayani Chunya, Ujenzi wa Madarasa kwa pesa za Boost pamoja na ujenzi wa Shule Mpya, upanuzi wa Hospitali ya wilaya pamoja na miradi mingine mingi
AAidha Mhe Masache amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya Kuhifadhi chakula cha Kutosha familia zao huku akiwataka kutokuwa na haraka kuuza ile ziada ya Chakula walichonacho kwani bei ya Chakula hiyo inaweza kuwa kubwa muda si mrefu hivyo watauza kwa bei kubwa hapo baadaye
“Niwaombe baba zangu, mama zangu, wazee wangu pamoja na vijana wenzangu, chonde chonde naomba tutunze chakula cha Kutosha kwani inawezekana huku mbeleni tatizo la Njaa likatukumba na wanaotaka kuuza ziazda ya Chakula walichopata wawe na subiri kidogo huko mbeleni kutakuwa na bei kubwa hivyo wakiuza muda huo inawasaidia hata kupata Mbolea kwaajili ya msimu ujao”
Ziara ya Mhe Bunge inahusisha viongozi Mbalimbali wa Chama na serikali ikiwa na lengo la kutua changamoto za wananchi hapo kwa hapo na kuzichukua changamoto ambazo zinahitaji mchakato wa kuzitatua ili kwenda kufuatilia katika mamlaka zinazohusika. Jumamosi ya Tarehe 29/7/2023 ni zamu ya Kata ya Chokaa ambapo mkutano wa kwanzan ni Kitongoji cha Sambilimwaya na Baddaye Mkutano mwingine utakuwa kijiji cha Kibaoni ambao utafanyika eneo la ofisi ya kijiji
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Kasaka (Mwenye shati jeupe na ameweka mikono yake nyuma) akimsikiliza Mkuu wa Shule ya sekondari Itewe Baada ya kutembelea kukagua mradi wa ujenzi wa Bweni
Mbunge wa jimbo la Lupa akiwasili eneo la Kikao kata ya Itewe ili kuzungumza na viongozi wa Chama na serikali kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya
Mbunge wa Jimbo la Lupa akipokea Cheti cha Pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Itewe baada ya kumalizika kikao cha ndani kabla ya kwenda kuzungumza na wananchi wa kata ya itewe katika kijiji cha Chunya Mjini
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache akicheza na wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) kutoka kijiji cha Sinjilili A baada ya kuhitimisha zoezi la kuzungumza na wananchi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.