Mbunge wa jimbo la Lupa Mhe. Masache Njelu Kasaka meishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeipatia fedha nyingi wilaya ya chunya katika sekta ya Afya, sambamba na kuleta gari la kubebea wagonjwa “Ambulance”
Ametoa shukrani hizo jana January 20, 2024 katika hafla fupi ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) llilotolewa na Serikali ya Awamu ya sita kwa uongozi wa Hospitali ya wilaya ya Chunya lengo likiwa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wilayani humo.
“kipekee nimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani ambavyo ameendelea kutupatia fedha katika sekta ya Afya amezungumza hapa Mganga mkuu wa wilaya ni zaidi ya Bilioni 2.5 zote zimekwenda katika ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Hospitali ya wilaya, vituo vya afya pamoja na Zahanati”
Mhe Masache amesema gari hilo litakuwa masaada mkubwa kwa wananchi wa Chunya kwani jiografia ya wilaya ya Chunya ni kubwa mno jambo linalopelekea ugumu kumfikia mwananchi aliyeko mbalimbali wakati huo huo kulikuwa na upungufu wa magari ya kubebea wagonjwa
“Ninyi mtakuwa mashaidi Chunya ni kubwa na imekuwa na changamoto ya magari ya wagonjwa na kutokana na ukubwa huu magari ambayo tulikuwa nayo yalikuwa hayatoshelezi na pia hayakuwa katika ubora mzuri zaidi” alisema Mhe. Masache
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Darison amesema mahitaji ya gari la kubebea wagonjwa yalikwa ni makubwa mno ukiinganisha na ukubwa wa jiografia ya wilaya ya Chunya, hivyo kupitia uwepo wa Gari hii ya kubebea wagonjwa wananchi watafikiwa kwa wakati pindi wapatapo changamoto ya Afya
“Gari hili litasaidia wagonjwa wetu kupata huduma kwa wakati na kupunguza usumbufu wa kupata hadha ya usafiri kwa muda ambao unakuwa unahitajika, aidha tunaendelea kumshuruku Mhe. Rais namna ambavyo ameendelea kutujali sisi kama Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa kutupatia watumishi” alisema Dr. Darison
Aidha Dkt. Darison Andrew amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia kwa kutoa fedha shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa majengo nane katika hospitali ya wilaya ya Chunya na fedha bilioni 1.1 kwa ajili ya madawa na vifaa tiba kwa sekta ya Afya wilaya ya Chunya, ambapo awamu iliyopita milioni 400 na kwa awamuhii milioni 700
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka akiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na Madaktari wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria kukabidhi rasmi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Uongozi wa Afya wilaya ya Chunya
Gari ya Kubebea wagonjwa (Ambulance) iliyokabidhiwa na Mhe Mbunge wa Uongozi wa sekta ya Afya wilaya ya Chunya mwishoni mwa Juma
Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa akizungumza na viongozi waliofika kwenye hafla ya kukabidhi gari ya kubebea wagonjwa kabla zoezi la Kukabidhi gari hiyo halijaanza
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.