Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka amechangia mifuko mia mbili na thelasini (230) ya Saruji katika kata ya Chalangwa ili kuungana na wananchi kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika huku akiwaahidi wananchi hao kuendeleo kuiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta fedha ili kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Jimbo la Lupa wakiwepo wananchi wa Kata ya Chalangwa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti leo tarehe 10/10/2023 wakati wa ziara yake ya kupokea na kutatua kero za wananchi katika mikutano miwili tofauti amesema yeye kama mtoto wa jimbo la Lupa lazima ashiriki kikamilifu kuhakikisha kero mbalimbali za wananchi zinatatuliwa ili wananchi waendelee na shughuli zao za kawaida za kujipatia kipato na hatimaye ujenzi wa Jamii na Taifa imara kwa kuimarisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
“Nimeona juhudi zenu za ujenzi wa Bweni katika shule ya Sekondari ya kata ya Chalangwa na mimi kama mwenzenu lazima niwaunge mkono tukamilishe ujenzi huo ili watoto wetu wapate mazingira mazuri ya kusoma hivyo nitachangia mifuko mia moja (100) ya saruji ili mwendelee na ujenzi huo. Na kwakuwa Afya ndio kila kitu maana bila uimara wa afya zetu basi hakuna kinachoweza kufanyika na pia nimeona juhudi zenu katika ujenzi wa wodi katika kituo cha afya cha Chalangwa lazima nishiriki kuimarisha afya za wanachunya nitachangia mifuko mia moja (100) kwenye kituo cha Afya”.
Mhe Masache amechangia mifuko 30 ili kuunga mkono ujenzi wa Josho katika kijiji cha Itumba kilichopo kata ya Chalangwa ili kutatua changamoto ya josho eneo hili ikiwa ni ombi kutoka Mwananchi wa eneo hilo alipopata nafasi ya kutoa kero yake mbele ya Mbunge wa Jimbo la Lupa alipotembelea kijiji hicho leo ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia suluhu zinazowekana kwa wakati huo na kuchukua kero zilizo nje ya uwezo wake na kuendelea kutafuta suluhu ili wananchi waendelee na shughuli za uzalishaji mali.
Mhe Diwani wa Kata ya Chalangwa Mhe Haji Chapa amesema wananchi wa kata ya Chalangwa wanaishukuru serikali kwa namna ambavyo fedha nyingi zimeletwa katika kata hiyo ingawa bado kuna changamoto mbalimbali kama vile Maji, umeme na daraja la izumbi hivyo amemwomba Mbunge wa Jimbo la Lupa kuendelea kuwapambania wananchi wa Chalangwa na Chunya Kwa ujumla wake ili changamoto hizo zipate suluhu kama ilivyo kwenye afya kwani uwepo wa kituo cha Afya Chalangwa umeleta suluhu ya Changamoto zote kwa upande wa Afya.
Fanuel Dickson Mbalamwezi, Samwel Wiston, Luciana Shonza, Mwakisole Edwin na Mawazo Jailos kwa niaba ya wananchi wengine wameishuru serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa kwa namna ambavyo wameendelea kutatua kero za wananchi wa Kata ya Chalangwa huku wakiendelea kuomba kusaidiwa kupata walimu katika shule za Msingi katika kata hiyo, maji ya uhakika pamoja na usimamizi wa Mbolea ya Ruzuku ili waweze kufanya vizuri katika kilimo msimu ujao.
Mbunge wa Jimbo la Lupa bado anaendelea na ziara ya kukutana na wananchi ili kuwapa mrejesho wa utekelezaji wa yale aliyotumwa kuyatekeleza lakini pia kuchukua kero na changamoto nyingine ili aendelee kutafuta suluhu kwana kwa kushirikiana na wnanchi na zile nyingine kuenda kuiomba serikali kupitia bunge kusaidia kuleta suluhu yake. Ziara itaendelea kesho kwa kata ya Ifumbo ambapo mikutano miwili itafanyika kuanzia kijiji cha Lupamaketi na baadaye kijiji cha Ifumbo
Mbunge wa Jimbo la Lupa (Katika aliyevaa suti ya Blue) akihutubia wananchi wa kijiji cha Chalangwa
Diwani wa kata ya Chalangwa Mh. Haji Chapa akizungumza kwa furaha mambo yaliyotekelezwa kwenye kata hiyo na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kumkaribisha bunge wa Jimbo la Lupa wakati wa ziara ya kuzungmza na wananchi wa Itumba
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Itumba Mwalimu Sadock Waiton Gallaakitoa shukrani zake kwa niaba ya Shule ya Msingi Itumba kwa Mbunge wa Jimbo la Lupa kwa namna alivyoshiriki katika kuchangia ujenzi wa majengo mbalimbali katika shule hiyo
Mbunge wa Jimbo la Lupa akieleza jambo wakati alipokuta na uongozi wa Jumuhiya ya watumia maji kata ya Chalangwa kabla ya kuanza mikutano ya ndani na mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya kuzungumza na wanancchi wa kata ya Chalangwa
Katibu wa umoja wa vijana wa wilaya ya Chunya Ndugu Mayeye akizungumza jambo kwenye kikao cha viongozi wa Jumuhiya ya watumia maji kata ya Chalangwa wakati Mbunge wa Jimbo la Lupa alipotembelea kata ya Chalangwa
Mbunge wa Jimbo la Lupa pamoja na viongozi wa jumuhiya ya watumia maji kata ya Chalangwa wakati wa Mazungmza yao kuhusu changamoto ya maji katika kata hiyo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.