Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewaagiza viongozi wa Serikali walioko kwenye vijiji na kata za Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuwaongoza na kuwasaidia Mafundi wazawa pamoja na wananchi wenye uwezo wa kuwa wazabuni wa vifaa mbalimbali kujisajili kwenye mfumo wa Nest ili waweze kunufaika kwa kutoa huduma kwa Serikali wakati wa utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao
Ametoa agizo hilo leo 10/12/2024 wakati kamati ya Usalama ilipokuwa inakagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Nkung’ungu inayojengwa kwa fedha shilingi milioni mia tano themanini na tatu kutoka Serikali kuu
“Ninyi watendaji wa vijiji na kata, walimu wakuu na wakuu wa Shule waongozeni Mafundi wazawa pamoja na wananchi wanaoweza kuwa wazabuni katika miradi mbalimbali wajiunge kwenye mfumo wa Nest ili waweze kuomba tenda ili kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo itapunguza baadhi ya usumbufu mnaokutana nao wakati wa utekelezaji wa miradi kwa kupitia mafundi wanaotoka mbali na eneo la ujenzi wa mradi”
Aidha Mhe Batenga ameonya kamati za Ujenzi kutopokea vifaa vyenye mapungufu au vibovu kwani vifaa vibovu ndio mwanzo wa kazi kukosa ubora huku akiwakumbusha kwamba ikibainika vifaa vyovyote vibovu vimepokelewa basi watawajibika
“Kamati msipokee vifaa/vitu vibovu, Naomba sana hilo. Na kama hamjaelewana mwambie aliyeleta vifaa vibovu kwamba aviweke pembeni mpaka vitakapokaguliwa. Tafadhari sana nimetoa tahadhari hii mapema kabisa maana atakayebainika tutagombana sana eneo hili” Aliongeza Mhe Batenga
Kaimu Mkurugenzi mtendaji Ndugu Cuthbert Mwinuka amesema Kuanzia tarehe 17/12/2024 kamati maalumu itapita kwenye kila mradi kutoa elimu ya namna ya kusimamia miradi inayotekelezwa ili kuongeza usimamizi na ufanisi wa utekelezaji wa miradi, ikiwa ni utekelezaji wa moja ya maagizo ya kamati ya usalama wilaya baada ya kukagua miradi kadhaa inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya
Kamati ya Usalama ya wikaya ya Chunya ikiongozwa na mwenyekiti wake Mkuu wa wilaya ya Chunya, imeanza Ziara leo 10/12/2024 ambapo miradi yenye thamani ya shilingi milioni mia nane kumi na saba (817,159,028) imekaguliwa huku ziara hiyo ikitaraji kuendelea kesho tarehe 11/12/2024 ambapo miradi mingine yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni mia sita (600,000,000) itakaguliwa
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Batenga (Aliyeshika karatasi Mkono wake wa Kulia) akizungumza Jambo wakati kamati ya Usalama ilipokuwa inakagua ujenzi wa Nyumba ya walimu (Two in one) shule ya Sekondari Kambikatoto
Mkuu wa wilaya ya Chunya akifafanua jambo wakati kamati ya usalama ilipokuwa inakagua ukarabati wa Bwalo la Chakula Shule ya Sekondari Lupa
Baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari Nkung'ungu, Kamati ya Usalama wilaya ya Chunya pia ilipita na kukagua mradi huo ambao mpaka sasa uko asilimia 65
Kamati ya Usalama ikipokea taarifa ya ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo Shule ya Msingi Mtande, Kamati imepongeza na kusema Ujenzi unaendelea vizuri
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.