Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Chunya kwamba Mhe Rais Samia Suluhu Hassan anatambua changamoto zote zinazowakumba wananchi wa Chunya na anazipatia Majibu Changamoto moja baada ya nyingine huku akirejerea Ujenzi wa Kituo cha Afya Kambikatoto, Ujenzi wa Shule ya Sekondari na sasa Utekelezaji wa mradi wa Maji unaotaraji kuanza hivi karibuni.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Kambikatoto leo tarehe 29/5/2024 baada ya kumkabidhi mkataba wa Utekelezaji wa Mradi huo Mhandisi Richard Juma kutoka Kampuni ya EquiplusCompany Limited inayotaraji kutekeleza mradi huo Mhe Batenga amewataka wananchi kuwa na Imani na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani changamoto zote zinapatiwa Suluhu kwa wakati
“Kurahisisha upatikanaji wa Matibabu ya Kibingwa Mhe Rais ametuletea madaktari Bingwa hapa hapa wilayani Chunya, Kituo cha Afya kimejengwa hapa Kambikatoto, Sekondari imejengwa hapa na wanafunzi tayari wanasoma hapa ndugu wananchi Mhe Rais Hajawafikia? Niwaombe muendelee kuiamini Serikali hii ya awamu ya sita na ndo maana leo Mradi wa maji unaanza kutekelezwa hapa kwenu” Amesema Mhe Batenga
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya Meneja wa RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga amesema Halmashauri ya wilaya ya Chunya imepokea fedha zaidi ya Bilioni tano ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ndani ya wilaya ya Chunya huku akisema miradi mingine imekwisha kamilika na mingine iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
“Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya wilaya ya Chunya tumepokea fedha bilioni tano na milioni mia tisa ambapo bilioni nne zimepelekwa wenye mradi wa Maji wa Matwiga wakati pesa zinazobaki zimepelekwa kwenye miradi mbalimbali ikiwepo uchimbaji wa visima katika vijiji kwa Bitimanyanga, Mafyeko, Mtanila, Lupa na Mamba na miradi ya Uchimbaji wa visima inatakiwa kuisha tarehe 30 juni” Amesma Mhandi Sanga
Mhandisi kutoka Kampuni ya Equiplus Company Limited Mhandisi Richard Juma kwa niaba ya Kampuni yake amesema wamejipanga kutekeleza mradi huo kwa ubora, ufanisi na mradi utatekelezwa ndani ya muda uliopangwa huku akiishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuiamini Kampuni hiyo katika kutekeleza mradi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde amewashukuru sana wananchi wa kata ya Kambikatoto kwa namna wanavyoshiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao huku akiwataka kufanya hivyo pia kwenye mradi maji unaotaraji kuanza kutekelezwa katika kata ya Kambikatoto.
Mradi wa Maji unaotaraji kutekelezwa katika kata ya Kambikatoto utagharimu fedha shilingi milioni mia tano tisini na tano, unajengwa na Kampuni inayoitwa Equiplus Company Limited ambapo utajengwa kwa miezi sita hivyo mradi huo utakamilika mwezi Disemba na utakapokamilika utahudumia wananchi wa kijiji cha Kambikatoto kwa asilimia mia moja
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga (Aliyavaa Shati la Drafti) akimkabidhi Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa Maji Mhandisi Richard Juma kutoka Kambuni ya
Equiplus Company Limited itakayotekelezaji ujenzi wa mradi wa maji Kambikatoto
Meneja wa RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga akizungumza Jambo wakati wa mkutano wa Hadhara Kambikatoto kabla ya Mkuu wa wilaya ya Chunya Kumkabidhi mkandarasi mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco Mwanginde akizungumza na wananchi wa kata ya Kambikatoto wakati wa Mkutano wa kumkabidishi Mkandarasi mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Kambikatoto
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga ( Wa kwanza Kushoto na amevaa shati la Drafti) akiwa pamoja na viongozi Mbalimbali wakipokea taarifa ya kisima ambacho kitatumika kugawa maji kwenye kijiji cha kambikatoto baada ya miundombinu yake kukamilika
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.