Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka waajiriwa wapya kufanya kazi kwa uadilifu wanapokuwa katika vituo vyao vya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali kwasababu wakifanya hivyo watakuwa wametekeleza azma ya serikali ya kuwatumikia wananchi wote bila kujali cheo, jinsi, nafasi na hata kipato cha mtu
Ameyasema hayo 18/09/2023 wakati wa mafunzo kwa waajiriwa wapya walio katika kada mbalimbali ambazo ni kada ya elimu, afya, utawala na mawasiliano yaliyotelewa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya uliopo jengo jipya la utawala ambapo jumla ya ya waajiriwa 190 wamenufaika na mafunzo hayo.
“Mmeajiriwa sasa kuwa watumishi wa serikali mkafuate taratibu kanuni na miongozo ya serikali na mkawe wavumilivu na kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo mtakutana nazo kwa kushirikiana na viongozi kwani serikali inawategemea sana mkafanye kazi kwa uadilifu mkubwa.” Alisema Mhe. Mwanginde
Mhe. Mwanginde pia amewatahadharisha waajiriwa wapya kuwa makini na mikopo kwani inaweza ikawasababisha wakawa na maisha magumu hivyo wanapaswa kujiandaa kabla ya kufanya maamuzi ya kuchukua mikopo ili mwisho wa siku isije ikawapa shida wakati wa kurejesha.
Nae Mkurugenzi Mtendaji ndugu Tamim Kambona amewataka waajiriwa wapya hao kuzingatia suala la nidhamu na kujiheshimu kama watumishi wanapokuwa kazini lakini pia hata katika jamii inayowazunguka wahakikishe wanashirikiana vizuri na watumishi wenzao katika vituo vya kazi na hata jamii inayowazunguka
Katika semina hiyo elekezi mada mbalimali zimefundishwa ikiwa ni pamoja na haki na wajibu wa mtumishi katika utumishi wa umma , Miiko ya watumishi wa afya , Huduma zinazotolewa na mfuko wa Taifa wa bima ya Afya pamoja na jinsi ya kujisajili katika mfumo wa MUKI.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa makundi ambapo kundi la kwanza kupata mafunzo hayo ilikuwa kada ya Elimu ambapo walimu 98 walipatiwa mafunzo na kundi la pili limejumuisha kada ya Afya, Utawala na mawasiliano jumla ya waajiriwa ambapo jumla ya watumishi wapya 92 wamepata mafunzo hayo, Na wawezeshaji katika mafunzo hayo ni Maafisa utumishi na utawala, Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya na Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ( NHIF)
Afisa utumishi na rasilimali watu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu John Maholani akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo elekezi kwa watumishi wa ajira Mpya
Baadhi ya watumishi wa kada mbalimbali (Ajira Mpya) Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakifuatilia semina elekezi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.