Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh. Maryprisca Mahundi amewataka vijana kutoka katika kata tatu za Sangambi, Chalangwa na Mbugani waliopata mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi wa vyoo bora kupitia mradi wa Ushirikishwaji vijana katika ujenzi wa vyoo bora kibiashara (YESB) kuwa chachu ya mabadilikokwenye jamii.
Maryprisca amasema kuwa jamii ikiwa na vyoo bora kutawaepusha na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na vijana hao waliohitimu mafunzo hayo wawe mabalozi wazuri katika kuhimiza na kuwapatia jamii elimu juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo bora.
Tazama picha zaid hapa chini
Picha ya pamoja ya Mh. Maryprisca Mahundi na vijana waliopata mafunzo ya ujasiriamali
Mkuu wa wilaya ya Chunya (nguo nyekundu),kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Chunya Bi. Sophia Kumbuli pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya YESB
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.