Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga amemshukuru rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta madaktari bigwa wa ugonjwa wa mtoto wa jicho katika hospitali ya Wilaya ya Chunya bila garama yoyote ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo
Kauli hiyo ameisema leo 19 Novemba 2024 katika Hospital ya Wilaya ya Chunya wakati alipowatembelea na kuzungumza na wagonjwa mbalimbali waliofika kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho inayodhaminiwa serikali kwa kushirikiana na shirika Hellen Keeler
Mh. Batenga amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muunganio wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta madaktari bigwa wa ugonjwa wa mtoto wa jicho katika Wilaya ya Chunya ambapo zaidi ya wagonjwa 500 wanatarajiwa kupatiwa matibabu.
“Namshukuru rais Samia, wataalamu na madaktari wetu na timu nzima kwa kutoa huduma bora za kibigwa za mtoto wa jicho, huduma hii sio mara ya kwanza hapa Chunya tayari ilishatolewa ambapo wagonjwa 466 walipatiwa matibabu na wameshapona na wanaendelea na shughuli zao za Uchumi, uzoefu ulionesha kwamba kuna kuna watu wengine hawakufikiwa na huduma hii hivyo wamerudi tena mara ya pili na watahudumu kwa muda wa siku tano na wanatarajia kuwahudumia wagonjwa 500” amesema Batenga.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew amewaeleza wagonjwa waliofika Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwaajili ya kupatiwa matibabu kuwa, huduma ya uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho inatolewa bure bila malipo yeyote, Vilevile chakula cha asubuhi, mchana na jioni nacho kinatolewa bure kwa wagonjwa pamoja na usafiri wa kuwafuata na kuwarudisha wagonjwa kwenye maeneo yanapotoka
Naye, Bi Olider Mwakipesile mkazi wa Kata ya Matwiga, amewashukuru madaktari kwa huduma ya matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho kwani amesumbuliwa na ugonjwa ugonjwa huo kwa muda wa miaka mawili tangu mwaka 2022 bila kupata matibabu yoyote kwasababu ya kukosa fedha za matibabu.
Omari Ukumbi mwananchi wa Wilaya ya Chunya ameishukuru serikali kwa kuwaletea huduma ya ugonjwa wa mtoto wa jicho bure bila malipo na kuwataka wananchi wengine wenye shida ya macho wajitokeze kupata matibabu hayo wanayotolewa Hospitali ya Wilaya ya Chunya.
Huduma hiyo ya kibingwa ya motto wa jicho itadumu kwa muda wa siku 5 ambapo imeanza kutolewa tarehe Novemba 18/ 2024 na kuhitimishwa tarehe Novemba 22/2024 katika Hospital ya Wilaya ya Chunya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akizungumza na wagonjwa mbalimbali waliofika katika Hospital ya Wilaya ya Chunya kwaajili ya kupata matibabu ya mtoto wa Jicho
Wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwaajili ya kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya mtoto wa Jicho wakiendelea kuhudumiwa.
Hatua za awali za matibubu zikiendelea kwa wagonjwa waliofika katika Hospital ya Wilaya ya Chunya kwaajili ya matibabu ya mtoto wa jicho
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.