Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasaka amewataka wananchi wa jimbo la Lupa waendelee kuiamini serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani mpaka sasa imeendelea kutekeleza ahadi zote zilizoahidiwa mwaka 2020 na bado inaendelea kutekeleza.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 05/10/2023 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nkwangu kwanza kuwapa mrejeso kuhusu Bunge la bajeti na kueleza shughuli mbalimbali zilizofanyika na ambazo zinaendelea kufanyika pamoja na kusikiliza kero za wananchi hatimaye kuzipatia suluhu kero hizo.
“Mimi na viongozi wenzangu hatujawaangusha na hatutawaangusha maana tukiwaangusha maana yake tumemwangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Mama Samia Suluhu Hassan jambo ambalo sisi watumishi wenu mliotutuma kuwasemeeni maeneo mbalimbali hatuwezi kufanya hivyo maana hata ninyi ni mashahidi kwamba ahadi tulizo ahidi tunaendelea kuzitekeleza”.
Akijibu kero mbalimbali za wananchi Mhe Mbunge amesema Wilaya ya Chunya imetengewa fedha zaidi ya Milioni mia nane kwaajili ya kununua vifaa tiba kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 hivyo Zahanati ya kijiji cha Nkwangu itakuwa ni moja kati ya wanufaika wa vifaa hivyo ili wananchi waendelee kupata huduma katika zahanati hiyo huku akiwata viongozi kuwapa mrejesho wananchi kuhusu fedha za maendeleo zinazoletwa na hata michango ya wananchi.
“Hakikisheni wananchi wanapata taarifa ya fedha za serikali zinazoletwa kujenga miradi mbalimbali pamoja na fedha zinazotokana na michango yao ili kuepuka usumbufu kwani wananchi wamekuwa wakilalamika kwamba wanachaga fedha lakini hawaoni kilichofanyika lakini ukifuatilia unakuta fedha hizo zimefanya mambo mazuri lakini wananchi hawajui”.
Diwani wa kata ya Upendo Mhe. Mh. Richard N. Itelekelo amemshukuru Mhe Mbunge kwa namna ambavyo ameendelea kuwa mstari wa Mbele kuwapigania wananchi wa wilaya ya Chunya hasa kata ya Upendo kwani miradi mbalimbali kama vile uchimbaji wa visima, ujenzi wa shule ya sekondari, ujenzi wa zahanati na mingine mingi inatekelezwa katika kata ya Upendo kwa fedha kutoka serikalini.
Awali akisoma taarifa kwa niaba ya wananchi mbele ya Mbunge wa jimbo la Lupa Mtendaji wa kijiji cha Nkwangu ndugu Andrew Msoya amesema kijiji kinakabiliwa na Chnagamoto mbalimbali zikiwepo Barabara, kukosekana kwa mawasiliano, Nyumba za watumishi waliopo katika kijiji hicho, vifaa tiba katika zahanati hiyo pamoja na vitanda na Friji la kutunzia chanjo kwaajili ya watoto jambo ambalo husababisha watoto wanaostahili kupata chanjo kukosa chanjo hiyo hivyo kuhatarisha maisha yao.
Mbunge wa jimbo la Lupa yupo katika Ziara yake ya kawaida kuwatembelea wananchi ili kuwapa mrejeso wa bunge la Bajeti lililotamatika mwezi juni, kusikiliza kero za wananchi na kutafuta suluhu na kueleza namna ambavyo serikali inaendelea kutekeleza majukumu yake ili kuleta maendeleo kwa wanachunya wakiwepo wananchi wa kijiji cha Nkwangu. Ziara hiyo itaendelea kesho tarehe 8/10/2023 kwa kata ya Mkola.
Wanacnhi wa kijiji cha Nkwangu wakiwa katika hali ya furaha na shangwe na wengine wakiwa wameinua juu matawi ya miti huku wakishangilia wakati wa mapokezi ya Mbunge wa jimbo la Lupa wakati alipotembelea kijiji hicho wakati wa ziara ya kuwatembelea wananchi wa Jimbo la Lupa
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache (aliyesimama, Mwenye shati la drafti ndogo) akiinamisha kichwa chake ishara ya kupokea kero ya vifaa tiba katika zahanati ya kijiji cha Nkwangu wakati umoja ya wanawake wa Chama cha mapinduzi walipowasilisha kero hiyo kupitia igizo fupo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.