MKUU wa Wilaya ya Chunya Mh. Mayeka Simon Mayeka Machi 24, 2022 amefungua Mafunzo kwa Makarani watakaotekeleza zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Mafunzo hayo yatawapa uwezo Makarani kufahamau namna nzuri ya kusanya taarifa za Anwani za Makazi na kuziingiza kwenye mfumo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mh. Mayeka amewataka makarani kusikiliza kwa makini mafundisho watakayopewa na wataalam ili waende kufanya kazi kwa uweledi mkubwa.
“Mtaenda kufanya kazi ya kuchukua taarifa na kuingiza kwenye mfumo, hivyo ni vyema kuhakikisha kile unachokifanya ni sahihi ili tuamini hata kazi nyingine zinazofuatia unaweza kuzifanya.
“Niwaombe sana fanyeni kazi hii vizuri huwezi kujua kuna kazi gani nyingine zinaendelea za kitaifa pengine ukifanya kazi hii itakupa sababu ya kufanya kazi nyingine.” Alisema Mh. Mayeka.
Kadhalika, Mayeka aliwataka makarani kuweka uzalendo na maslahi ya taifa mbele, kwani jukumu walilokabidhiwa ni kubwa na la kitaifa, hivyo makosa watakayoyafanya Chunya, watasababisha yasomeke kwa taifa zima.
“Nyinyi ni vijana kama nilivyotangulia kusema tunawaamini na mtafanya kazi hii ya kuingiza taarifa kwa uzalendo mimi sina wasiwasi kabisa.” Mh Mayeka.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndg Curthbert Mwinuka amewasisitiza makarani kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa
“Hakikisheni mnazingatia vigezo vyote vinavyotakiwa au mtakavyoelekezwa hapa kwa ajili ya kutekeleza zoezi hili, sitarajii mkafanye namna ambayo hamjaelekezwa na sitarajii kuona maeneo mtakayopangiwa mruke nyumba hata moja.” Aklisema Mwinuka.
Aidha, Mwinuka aliongeza kwa kuwakumbusha umuhimu wa zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi na kuwataka makarani hao kufanya kazi kwa weledi bila ya kuleta dosari yoyote wakijua kabisa kuwa wanatumia rasilimali fedha za Serikali.
Washiriki wa Mafunzo ya Anwani za Makazi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.