Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasaka amesema kuridhia kwa azimio la Tanzania kuhusu mkataba wa kimataifa wa Nishati Jadidifu IRENA utaleta manufaa kwa nchi huku akibainisha kwamba nchi nyingine jirani zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda na Nchi nyingine za SADEC zilizoweza kuridhia mkataba huo mwaka 2011 wameendelea kufanya vizuri na manufaa wameyapata.
Mhe Masache ameyasema hay oleo tarehe 31/10/2023 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Azimio la Tanzania kuhusu kuridhia Mkataba wa wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadididfu IRENA.
“Baada ya muda mrefu wa kujiridhisha kuhusu mkataba huu sasa umefika muda muafaka wa kuona namna iyo nzuri bunge letu tukufu kwa maana ya watanzania turidhie mkata huu ili wananchi wetu waweze kufaidika”.
Aidha Mhe Masache ameshauri vyuo vyetu vya ndani ya Nchi kikiwepo Chuo Kikuu cha Sanyansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) kuongezewa uwezo ili viweze kutoa mafunzo yanayohusu nishati Jadididfu jambo litakalokuwa suluhu ya kupata wataalam hivyo kujipatia ajira katika uga huo wa Nishati Kadidifu.
“Lakini pia kupitia vyuo vyetu vya ndani tayari imeshasemwa hapa kwamba tunao DIT na Arusha Technical College lakini sisi kama kamati tuliiambia serikali tuweze kuongeza Chuo cha MUST pale Mbeya ili waweze kutoa kozi hizi itatusaidia kupata wataalamu wa kutosha”
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Kasaka akichangia azimio la Mkataba wa Nishati kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea jijini Dodoma
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.