Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Mayeka Simon Mayeka amepokea msaada wa mashuka wenye thamani ya sh. 627,000 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste {CPCT} Wilaya ya Chunya.
Hafla ya kukabidhi mashukahayo imefanyika leo Desemba 13, 2021 katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya na kushirikisha viongozi mbalimbaliwa CPCT Chunya.
Mayeka amewashukuru Viongozi wa CPCT Wilaya ya Chunya kwa msaada huo ambapo amesema, wamefanya jambo kubwa sana kwani mashuka nimahitaji muhimu kwa wagonjwa kwasababu yamekuwa yakitumika kila siku.
“Mimi nashukurukwa support hii mliyotoa, kwani Serikali na makanisa tumekuwa tukifanya kazi kwa miaka mingi sana. Mna Shule, Vituo vya Afya na Hospitali hivyo hiki mnachokifanya mmekuwa mkifanya miaka yote.” AmesemaMayeka.
Hatahivyo Mkuu wa Wilaya ameuhakikishia Uongozi wa Umoja wa makanisa ya Kipentekoste {CPCT} kuwa mashuka waliyoyatoa yatakwenda kufanya kazi kama walivyo kusudia, pia amewaomba wapeleke salam kwa waumini kuwa walichokifanya ni ibada.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Wilaya ya Chunya, Askofu Hansi Mwakibete amesema, msaada waliotoa ni mashuka 83 yaliyo gharimu kiasi cha sh. 672,000.
Amesema CPCT inaunga mkono juhudi za Viongozi wa Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali na kwamba wanatambua umuhimu wakutoa msaada ili wananchi waendelee kupata huduma bora.
Askofu Mwakibete aliongeza kwa kusema kuwa, utoaji wa misaada kwawasiojiweza na taasisi mbalimbali ni sehemu ya majukumu ya Makanisa ya Kipentekoste, hivyo niwajibu wao kufanya hivyo.
“Tumekuja hapa sio kwa bahati mbaya, nimoja ya majukumu yetu, tulikaa kwenye vikao kama Viongozi na Washirika tulio na wajibu katika jamii tukaona tutoe mchango kidogo.
“Tumelengae neo hili nyeti ambapo washiriki wetu pamoja na ndugu zetu wapo wanapata msaada.” Amesema Askofu Mwakibete wakati wakikabidhi mashuka hayo kwa Mkuu wa Wilaya katika wodi ya wazazi Hospitali ya Wilaya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.