Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha Majengo yanayojengwa katika Hospitali ya wilaya ya Chunya mbayo yapo hatua za mwisho yaanze kutumika ifikapo Mei 25 ili lengo la serikali la kuwapatia huduma wananchi wake litimie
Ametoa maelekezo hayo tarehe 26/4/2023 alipokagua mradi wa upanuzi wa Hospital ya wilaya ya Chunya na baadaye kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa Hospitali hiyo ambapo majengo mbalimbali yanajengwa ikiwepo Jengo la wagonjwa wa Nje (OPD), Wodi ya wanaume na wodi ya wanawake, Jengo la upasuaji, Jengo la Mama Ngojea na majengo mengine.
“Nimezungmza nao, nimewambia kwamba kufika tarehe 25/05/2023 majengo haya yaanze kutumika haya ya upasuaji ili wakinamama na kinababa wenye changamoto za uzazi basi waanze kupata huduma katika majengo haya. Na tumshukuru mweshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuleta pesa zaidi ya Bilioni 1.4 katika awamu mbalimbali ili kuendelea kuleta huduma kwa wananchi”
Mkuu pia amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya kusimamia ujenzi wa miradi hiyo ili iendelee kuleta tija kusudiwa kwa wananchi
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka Saimon Mayeka amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwamba ataendelea kumuwakilisha mweshimiwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pamoja na Mkuu wa Mkoa katika kuhakikisha miradi inasimimiwa ipasavyo ili ilete tija iliyokusudiwa kwa watanzania wanoishi wilayani Chunya
“Kitu ambacho naweza kukuahidi ni usimizi wa miradi hasa fedha zilizokuja kwenye ujenzi wa hospitali hii, .Nichukue fursa hii kumshukuru mweshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuendelea kuleta pesa za miradi mbalimbali ikiwepo fedha za upanuzi wa hospitali yetu ya wilaya ya Chunya tofauti na historia inavyoeleza kwamba hospital hii hapo awali ilikuwa zahanati”
Naye Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe. Ramadhani Shumbi amesema pamoja na miradi yote inayoendela kujengwa katika wilaya ya chunya wataisimamia ipasavyo kuhakikisha inajengwa kwa ubora stahiki
“Pamoja na miradi yote inayoendela hapa chunya, nikuhakikishie kwamba kama Halmashauri ya wilaya tuko vizuri na tutaendela pokea pesa za miradi na kuisimamia vizuri, Niseme tu wilayani Chunya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa vizuri. Na wananchi wa chunya wako pamoja na Rais pamoja na wewe katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana”
Mkurugenzi Mtednaji halmashauri ya wilaya Ndugu Tamim Kambona amesema kama Halmashauri wataendelea kutenga fedha pale panapobidi ili kuendela kujenga maeneo watakayoona inafaa yajengwe Na tunamshukuru Mweshimiwa Rais kwa mwaka ujao ametutengea fedha zaidi ya Milioni 800 kwaajili ya kuendeleza ujenzi katika hospitali ya wilaya ya chunya.
Awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya Daktari Darison Andrew ameeleza hatua mbalimbali ambazo hospitali imekuwa ikichukua kuhakikisha miundombinu inaboreshwa ambapo moja ya juhudi ni andiko la mradi iliyopelekea UNICEF kufadhiri ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwepo jengo la Mama Ngojea
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hospitali imeendela kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha miundombinu ya hospitali, Kupitia UNICEF 2021 walitusaidia Kuchimba maji, 2022/2023 wametusadia kujenga majengo mbalimbali pamoja na kukarabati majengo kadhaa hapa katika hopspitali yetu ambapo gharama yake inakadiriwa kuwa bilioni moja na milioni mia mbili”
Kilele cha sherehe za Maadhimisho ya siku ya Muungano ambayo hufanyika kila tarehe 26/4 ya kila mwaka, kwa mwaka huu ilifanyika wilayani Chunya Kimkoa mabapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera. Kabla hajafika katika viwanja vya Shule ya Msingi Bwawani ambapo maadhimisho hayo yalifanyika Mkuu wa Mkoa alikagua uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa katika kata ya Mbugani na baadaye alitembelea hopsitali ya wilaya ya Chunya ambapo baada ya kukagua ujenzi unaoendela hospitalini hapo, aliweka jiwe la msingi la upanuzi wa hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera mwenye Miwani akizungumza jambo na Watendaji wa Halmashauri wakati akikagua Ujenzi wa majengo unaoendelea kwenye Hospitali ya wilaya, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka mwenye suti nyeusi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera akikata utepe kuashiria Upanuzi wa Hospitali ya wilaya ya Chunya
Mhe. Juma Z. Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Akipanda Mti (Mparachichi) katika Hospitali ya wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.