Afisa Mwandikishaji jimbo la Lupa Wakili Athuman Bamba ametoa rai kwa Waandikishaji wasaidizi wa Vituo na Waendesha vifaa vya Bayometric kuyatumia vizuri mafunzo waliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuendelea kupitia rejea mbalimbali walizopewa kwani mafunzo hayo ndio zana za kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vyema.
Ametoa rai hiyo leo Tarehe 24/12/2024 wakati akifunga Mafunzo ya siku mbili kwa Waandikishaji wasaidizi wa Vituo na waendesha vifaa vya Bayometriki yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo).
“Ninatoa Wito kwenu kuendelea kutumia muda wenu wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote mliyopewa ili kuongeza uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukum yenu katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura kwani Mafunzo mliyopewa ndio dhana ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi.”amesema Wakili Bamba
Aidha Wakili Bamba amewaambia Waandishi wasaidizi wa Vituo na waendesha vifaa vya bayometriki kuwa wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria , kanuni, miongozo na maelekezo yaliyotolewa na Tume ili kazi ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura ikatendeke kwa uadilifu na haki.
Naye Mwenyekiti wa mafunzo hayo Mwl.Isakwisa Kaminyoge kwa niaba ya washiriki wa Mafunzo hayo ameishukuru timu ya wataalam kutoka Tume , Maafisa wa Jimbo na Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kwa mafunzo waliyotoa pamoja na kuwaasa washiriki hao kwenda kufanya kazi waliyopangiwa kwa uaminifu, uadilifu na weledi mkubwa kwani wameaminiwa.
Mafunzo ya siku mbili kwa Waandikishaji wasaidizi wa Vituo na Waendesha vifaa vya Bayometriki yalijikita katika mada za ujazaji wa fomu mbalimbali zitakazo tumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura, fomu za kiapo, pamoja na mafunzo ya nadharia na vitendo juu ya namna ya kuandikisha wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kujiandikisha Wapiga kura (voters registration system ,VRS) ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura litakalo anza Tarehe 27/12/2024 na kutamatika Tarehe 2/1/2025.
Afisa Tehama kutoka Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi ndugu Overblessing Msuya akielezea vifaa mbalimbali vilivyomo katika BVR KIT wakati wa mafunzo kwa waandishi wasaidizi wa vituo na waendesha vifaa katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ( Sapanjo).
Mmoja ya washiriki wa mafunzo bi Nelly Magasha akiwaeleza washiriki wengine namna vifaa mbalimbali vinavyounganishwa.
Waandikishaji wasaidizi wa vituo na waendesha vifaa vya Bayometriki wakiendelea kufanya mazoezi juu ya matumizi ya vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura.
Waandisjhi wasaidizi wa vituo na waendesha vifaa vya Bayometriki wakifuatilia mafunzo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Sapanjo).
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.