Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Chunya kupitia kamati yake ya Fedha, Uongozi na Mipango imeagiza kuwakata fedha mafundi wanaoshindwa kusimamia vema Saruji wakati wanapotekeleza miradi mbalimbali ya Serikali jambo linalopelekea miradi kutokukamilika au kutumia kiwango kikubwa cha Saruji kuliko matarajio ya awali jambo linaloongeza gharama za utekelezaji wa miradi husika
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Daharia katika Shule ya Sekondari ya Isenyela mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Bosco Said Mwanginde ameiagiza kamati inayosimia mradi huo kuhakikisha Fundi anayetekeleza mradi huo anakatwa fedha ili kufidia Saruji iliyopotea kwa uzembe jambo ambalo halikubaliki
“Fundi kwanini unaacha Saruji hii inapotea namna hii? Kwanini hauchekechi mchanga wakati unapotaka kuchanganya na saruji tayari kwa kupiga ripu?, Hauoni kama kuna upotevu mkubwa wa Saruji tangu uliopanza kule mpaka hapa? Sasa kamati mnaosimamia mradi mkateni fundi kiasi cha Fedha ili kufidia Saruji hii iliyopotea kwa uzembe maana haiwezekana Saruji inapotea kwa namna hii” Amesema Mhe Mwanginde
Aidha Mhe Mwanginde ameagiza Fundi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Mabweni katika Shule ya Sekondari Sangambi kuhakikisha anazingatia muda aliopewa kutekeleza mradi huo kwa mujibu wa mkataba wake huku akiwataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanasimamia ubora na viwango vya utekelezaji wa mradi huo hatua kwa hatua
Wajumbe wa Kamati hiyo kwa nyakato tofauti wamepongeza kwanza Serikali kuendelea kuleta fedha katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambapo miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa lakini usimamizi unaofanywa na watalaamu wa Halmashauri wakishirikiana na kamati mbalimbali zinazotokana na wananchi waliopo kwenye maeneo ambako miradi hiyo inatekelezwa
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeanza ziara yake ya kawaida leo ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambapo Miradi yenye thamani ya Zaidi ya bilioni mbili imekaguliwa kwa siku ya kwanza, huku ziara hiyo ikipangwa kuendelea kwa siku ya pili tarehe 4/1/2024
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya akiongoza kamati hiyo kukagua ujenzi wa Mabweni katika Shule ya Sekondari Sangambi mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.