Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kupitia Mkoa wa Mbeya ndugu Ndele Mwaselela amesema viongozi wa Wilaya ya Chunya wametekeleza kwa vitendo maagizo matano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Pongezi hizo alizitoa wakati akizungumza na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya Septemba 2, 2024 huku akisema, Rais Samia alifika Chunya Agosti, 6 mwaka 2022, akihutubia mkutano wa hadhara, Rais alitoa maagizo matano ikiwemo kuziba miaya ya upotevu wa fedha na kukusanya mapato ili kuwaletea wananchi maendeleo.
“Rais Samia, alitoa maagizo matano ambayo kimsingi yote yametekelezwa kwa vitendo na Viongozi wa Wilaya ya Chunya, hongereni sana kwa kazi nzuri muliyoifanya” alisema Mwaselela.
Pamoja na mambo mengine Mwaselela amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kwa kusanya fedha vizuri jambo linalopelekea utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuwa halisia.
“Kwenye kukusanya mapato nimeambiwa hapa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imevuka lengo kwa kusanya asilimia 150 na kuziba mianya ya upotevu wa fedha kwa kulipa na kukusanya fedha kupitia mfumo” alisema Mwaselela.
Aidha Mwaselela amesema, Rais aliagiza ujenzi wa stendi mpya kubwa na ya kisasa Chunya, ambapo sasa Halmashauri ya Wilaya Chunya imeshatenga Shilingi Bilion 2.2 kwaajili ya stendi hiyo na Mkandarasi ataingia mkataba wa ujenzi wa Stendi hiyo siku ya Jumatatu, Septemba 9, 2024.
“Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imetenga kiasi cha shilingi Billion 2.2 kujenga stendi ya kisasa na itajengwa ndani miezi tisa hadi kukamilika na stendi hiyo itajengwa Itewe karibu na sheli ya LY” amesema Mwaselela.
Mheshimiwa Mwaselela ameongeza kuwa, agizo lingine ilikuwa ni uboreshwaji wa miundombinu na kununua vifaa tiba vya Hospitali ya Wilaya ya Chunya ambapo fedha za zilishafika na tayari kazi imefanyika.
“Serikali ilileta bilion 1.7 kwaajili ya kununua vifaa tiba na kuboresha miundombinu ya Hospitali ambapo Billioni 1.1 ni vifaa tiba na milioni mia sita ilikuwa ni kuboresha miundombinu”
Agizo la tano ilikuwa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Chunya, ambapo Mwaselela amesema asilimia 65 maji yanapatikana kwenye Wilaya hiyo.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Chunya, mhandisi Elineno Sanga amesema mpaka ikifika mwezi Mei mwakani maji yatafika kwa wananchi kwa asilimia 85 na lengo la kufikia asilimia 100 linaendelea kufikiwa.
Wakati huo huo wananchi waliiomba Serikali kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji, ujenzi wa barabara, ujenzi wa kituo cha polisi, na kutengenewa maeneo ya uchimbaji wa madini ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana na kina mama wa Wilaya ya Chunya.
MNEC aliwaahidi wananchi wa Wilaya ya Chunya kuwa, Chama cha Mapinduzi kimesikiliza na kimezichukua changamoto zote zilizoibuliwa na kwenda kuzifanyia kazi kwa haraka na kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM taifa Mkoa wa Mbeya ndugu Ndele Mwaselela akicheza na wananchi pamoja na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipotembelea kitongoji cha Itumbi kwaajili ya Kuzungumza na Wananchi wa kitongoji hicho.
Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa ndugu Ndele Mwaselela alipokuwa akisikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Itumbi. kata ya Makongolosi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.