Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mayeka S. Mayeka amewaasa na kuwataka maafisa usafirishaji wenye tabia ya kujihusisha na mapenzi na wanafunzi kuacha mara moja kwani madhara ya tabia hiyo ni makubwa kwa mtuhumiwa, mwanafunzi na hata jamii kwa ujumla
Ameyasema hayo wakati akizindua mashindano ya mpira wa miguu yanayoraji kufanyika katika uwanja wa mpira wa Miguu sababa yanayojulikana kama Mayeka usalama Cup, aliyoyaandaa kwa lengo la kuhamasisha watu kujifunza elimu ya usalama kwanza kwa maafisa usafirishaji na baadaye abiria na wananchi wengine wa wilaya ya Chunya
“Mtu anayekutwa na hatia ya kumpa Mimba mwanafunzi anaweza kupata kifungo cha maisha au miaka 20 niwaombe sana tuwalinde wanafunzi wote kwa pamoja na tuwaache watimeze ndoto zao” alisema Mhe Mayeka mkuu wa wilaya.
Pia Mhe Mayeka amewataka maafisa usafirishaji hao kujiepusha na vitendo viovu vinavyoweza kusababsha kupata kifungo cha maisha au adhabu mbalimbali jambo linaloweza kuathiri kazi zao pamoja na familia
“Baadhi yenu mmehusishwa na matukio mabaya ya uporaji, unyanganyi, ujambazi na utoroshaji wa dhahabu na wengine wamekamatwa wakibeba nyara za serikali kama meno ya Tembo, mbao na mkaa hayo yote ni mambo mnayopaswa kuwa makini” Alisema Mhe Mayeka
Aidha Mhe Mayeka amewataka Maafisa usafirishaji hao kusoma mwenendo ya wateje wao kwani maafisa usafirishaji hao wamekuwa wakibeba wateja wengi na wenye tabia mbalimbali hivyo ni vyema kuwa makini na wateja hao ili kuepuka kuingizwa kwenye hatia lakini pia kuhatarisha hata maisha yao wao wenyewe
Kwa uande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya chunya Ndugu Tamim Kambona amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri inatarajia kujenga kitua cha Radio ‘CHUNYA FM’ ili kuweza kuitangaza vyema Halmashauri ya wilaya ya Chunya ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa mbalimbali zilipo katika sekta ya Michezo wakati huo akisema ujenzi wa uwanja wa michezo uko hatua mbalimbali za ujenzi na ukikamilika utasaidia kupunguza adha ya viwanja Chunya
“Tunatarajia kwa mwaka ujao tutajenga redio ya kwetu ya halmashauri ya wilaya ya chunya ili tuweze kuitangaza Chunya yetu, sambamaba na hilo ujenzi wa uwanja wetu wa mpira unaendelea ingawa kuna kususa sua kidogo kutokana na changamoto za kimfumo lakini mara itakao rejea tutaendelea na zoezi lile lakukamilisha kwa hatua za mwisho ili tuweze kutengeneza Eneo la kuchezea (Pitch)”.
Mashindano hayo yanayotaraji kuhusisha timu nne kutoka kwa maafisa usafirisha, yatadumu kwa wiki moja mpaka kupatikana kwa msindi . Michezo iliyohusika katika ufunguzi ni pamoja na kuvuta Kamba, kukimbiza kuku pamoja na Mpira wa miguu ambapo timu ya Madereva Bajaji na Madereva bodaboda walitoka suluhu ya bila kufungana katika Mchezo huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamimu Kambona akizungumza na Hadhara ilyojitokeza wakati wa ufunguzi wa Mayeka Usalama Cyp mwisho mwa juma katika viwanja vya sabasaba Chunya
Mkuu wa wilaya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka akikagua timu wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Mayeka Uslama Cup mwishoni mwa juma
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka akigawa vifaa kwa moja ya timu zitakazoshiriki katika ligi ya Mayeka Usalama Cup inayotaraji kuchezwa wilayani Chunya hivi karibuni
Timu zikiendelea na mchezo wa Ufunguzi wa Ligi ya Mayeka Usalama Cup inayotaraji kuchezwa hivi karibu wilayani Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.