Maafisa lishe Wilaya ya Chunya wameagizwa kushirikiana na Maafisa Afya wakati wanapofanya ukaguzi na kuangalia usalama wa vyakula kwa mama ntilie ili waweze kutoa ushauri wa kitaalamu na mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika masuala mazima ya Lishe .
Maagizo hayo ameyatoa Afisa Mifugo Wilaya ya Chunya Dr Benedicto Matogo kwaniaba ya Mwenyekiti wa kamati ya lishe ambaya ni Mkrugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya leo Octoba 31/2024 wakati wa kikao cha Kamati ya lishe robo ya kwanza kilichoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
“Mjitahidi kuambatana na kushirikiana na Maafisa afya wanapokuwa wanafanya ukaguzi wa chakula na kuangalia usalama wa mazingira ya utayarishaji wa vyakula kwa mama ntilie ili muweze kutumia nafasi hio kutoa elimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya lishe na namnna ya kuandaa vyakula kwa kuzingatia makundi ya vyakula” alisema Dr Matogo.
Aidha ametoa rai kwa Wajumbe wa kamati ya Lishe kuhakikisha wanatekeleza yale yote waliyokubaliana katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kutekeleza mapango kazi ambao kila idara imejipangia kutekeleza juu ya lishe lakini pia kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha unaokuja wanakumbuka kuzitengea bajeti shughuli za lishe ambazo ni za muhimu ili ziwezwe kutekelezeka.
Pia amewaataka Maafisa kilimo waliopo ngazi ya kata kuhakikisha wanashirikiana na wakuu wa Shule katika maeneo yako ili kuhakikisha maeneo yote yaliyoytengwa na shule kwaajili ya shughuli za kilimo yanalimwa na yanapandwa mazao lishe ili kurahisisha upatikanaji wa chakula shuleni.
Naye Afisa lishe Wilaya ya Chunya bi Rehema Hiluka amewaomba idara ya elimu Msingi na Sekondari wanapokuwa wanafanya ufwatiliaji kwenye Shule zao wafwatilie pia Suala la ulaji wa chakula kwa wanafunzi wanapokua Shuleni lakini pia kukagua stoo ambazo wanahifadhia chakula ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula shuleni ikiwa ni adhima ya serikali kuhakikisha watoto wote wanapata chakula wanapokuwa Shuleni.
Kikao cha kamati ya Lishe robo ya kwanza kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba kimeambatana na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji kutoka katika idara ya Lishe, Idara ya elimu ya awali na msingi,Idara elimu Sekondari,Idara ya Kilimo na Mifugo na Idara ya Maendeleo ya Jamii ambapo katika taarifa hizo suala la uhamasishaji na elimu kwa wananchi juu ya masuala ya lishe limekuwa ni kipaumbele chao.
Afisa lishe Wilaya ya Chunya bi Rehema Hiluka akielezea namna ambavyo masuala ya Lishe yanatekelezwa katika ngazi za Kata wakati wa kikao cha kamati ya Lishe robo ya kwanza Julai hadi Septemba kilichoketi katika. Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Wajumbe wa kamati ya Lishe wakiendelea kupitia taarifa za idara mbalimbali zinazotekeleza afua za lishe wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya mwezi Julai hadi Septemba kilichoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Afisa elimu watu wazima na elimu nje ya Mfumo halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mwl Lukelo Mng'ong'o akisoma taarifa ya utekelezaji afua za lishe idara ya elimu Msingi na awali katika kikao cha kamati ya lishe.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.