Katibu tawala wa wilaya ya Chunya Ndugu Anaklet Michombero amewataka na kuwahimiza wanachama wa Vyama mbalimbali vya Ushirika vilivyo wilayani Chunya kuhakikisha wanalinda Umoja katika vyama vyao kwani mgawanyiko huleta mtafaruka na wakati mwingine kukosa umoja kunaweza kuhatarisha Vyama vyao.
Ametoa kauli hiyo leo wakati alipoaalikwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Msingi cha Ushirika Mtanila uliofanyika leo tarehe 6/12/2024 kwenye Ukumbi mdogo wa Ghala la Mtanila ambapo pia aligawa vifaa mbalimbali kama vile Kompyuta, Mashine ya kudurufu karatasi, vitanda, meza, dawati na viti vilivyonunuliwa na Chama hicho kwa lengo la kuigusa jamii yao inayowazunguka.
“Niwaombe muendelee kuwa wamoja na kwakufanya hivyo mtaendelea kuzalisha kwa faida kiasi cha kupata faida ambayo mnaweza kurudisha kwa Jamii kama mlivyofanya leo, Niwaombe sana lindeni umoja huu, Niwakumbushe mara zote mgawanyiko husabishwa na mambo makubwa mawili moja watu wanaotaka madaraka ambayo wanaweza wakawa wameyakosa kwenye chama hiki hivyo huanzisha vyama vingine ili wapate vyeo lakini sababu nyingine ni madeni, niwambie ukikimbia na Deni utalipa hata ukiwa Chama kingine” Amesema Michombero.
Naye Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Cuthberth Mwinuka awali akimkaribisha Mgeni rasmi amepongeza utulivu na juhudi ya wanachama wa Chama cha Msingi cha Mtanila ndiyo msingi wa mambo makubwa na Mazuri yanayofanywa na Chama hicho kwani kupitia utulivu wao wanajihusisha moja kwa moja kwenye uzalishaji.
Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tumbaku CHUTCU Ndugu Juma Shinshi amesema Mtanila ni chama kilichoshika nafasi ya kwanza kwenye uzalishaji wa Tumbaku kwa Msimu uliopita ambapo walizalisha tani milioni moja laki tano amewapongeza Chama hicho kwa kuzingatia ubora kwani katika upangaji wa viwango vya ubora Chama hicho kilikuwa nafasi ya nne.
Mwenyekiti wa Chama Cha msingi cha Ushirika cha Mtanila Ndugu Isaya Daniel Husen amesema wao kama Chama ni kawaida kutoa vitu mbalimbali kwa Jamii inayowazunguka kwani Mbali na vifaa vilivyotolewa leo, Chama hicho tayari kimefanya shughuli mbalimbali kwa jamii ya Mtanila ikiwepo ujenzi wa vivuko, Fursa kwenye kituo cha Afya na nyingine huku akisema kwasasa wamekubaliana kujenga wodi kwenye kituo cha Afya cha Mtanila.
“Kwasasa tumekubaliana kushiriki katika Shughuli mbalimbali za Ujenzi wa Wodi kwenye kituo cha Afya cha Mtanila ambapo kwa kuanzia tulitoa tripu kumi za mawe na kwasasa tumeruhusu matrekta yetu ya Chama Cha Mtanila Amcos kutumika kwenye shughuli za Ujenzi wa kituo hicho mpaka kitakapokamilika” Amesema Isaya.
Walimu wanufaika wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Chama cha Msingi cha Mtanila wamesema vifaa hivyo vitasaidia sana kupunguza changamoto zilizokuwepo maeneo mbalimbali, huku wakiwataka vyama vingine vilivyopo maeneo yao kuiga namna Chama hicho kilivyoona umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu jambo linalosaidia kuinua taaluma katika jamii
Chama Cha Msingi cha ushirika cha Mtanila kimefanya mkutano wake wa mwaka leo tarehe 6/12/2024 huku lengo kubwa likiwa ni kupitia utekelezaji wa makubaliano ya mkutano uliopita na kuweka mipango kwaajili ya Msimu wa kilimo unaoendelea na lengo likwa ni kufika tani Zaidi ya milioni mbili
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Chunya Ndugu Cuthberth Mwinuka akizungumza Jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Msingi cha Ushirika Mtanila Mapema leo
Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi cha Ushirika Mtanila Ndugu Isaya Husen akizungumza Jambo wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Chama Hicho yliofanyika mapema leo tarehe 6/12/2024
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Msingi cha Ushirika Mtanila wakisiskiliza maelezo kutoka kwa katibu Tarafa wa Tarafa ya Kipembawe Ndugu Kasim kirondomara wakati wa Mkutano wao wa mwaka ulioketi leo tarehe 06/12/2024
Wanachama wa Chama Cha Msingi cha Ushirika cha Mtanila wakipitia na kufuatilia kwa makini kila jambo linaloendelea kwenye mkutano wa mwaka wa Chama hicho ulioketi mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.