Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava amekabidhi leseni 11 za uchimbaji madini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chunya ndugu Tamim Kambona kwaajili ya kuwezesha Vijana kuchimba Madini kwa vitalu vyenye ukubwa wa ekari 151.8 vyenye gharama ya zaidi ya millioni sita vilivyopo msitu wa hifadhi wa Mbiwe kata ya Matundasi.
Akizungumza kwenye Mkesha wa Mwenge wa uhuru uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Makongolosi Agosti 24 mwaka huu, Mzava alisema kuwapatia leseni wachimbaji wadogo ni kurasimisha na kuongeza mnyororo wa thamani kwa vijana walioamua kujiajiri kupitia sekta hii ya madini.
“Ninyi viongozi wetu wa Wilaya mmetafsiri maono ya Mhe. Rais kwa vitendo kwa kuwapatia leseni kundi hili la vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli ya uchimbaji na hii ndio dhana ya uwezeshaji Vijana kiuchumi” alisema Mnzava.
Mzava aliwahimiza Viongozi wa Wilaya kuwawezesha mitaji wachimbaji wadogo kupitia kundi la vijana ili kuongeza mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini ambayo ni chanzo kimojawapo cha kuingiza mapato kwenye Wilaya hiyo.
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii, Bi Marietha Mlozi akisoma taarifa ya mpango maalum wa urasimishaji wa wachimbaji wa dogo katika sekta ya madini kwenye sherehe za Mwenge alisema, vijana watapata manufaa mbalimbali ikiwemo kujiajiri na kuweza kuajiri vijana wengine na kujiongezea kipato.
“Kupitia Programu maalum ya urasimishaji kwa wachimbaji wadogo kutawawezesha vijana hawa kunufaika moja kwa moja na rasirimali za Taifa na kuwezesha kuwa na maeneo ya uhakika ya uchimbaji wa madini” alisema Mlozi
Mlozi aliongeza kuwa, mpango wa urasimishaji kwa wachimbaj utawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu pamoja na kujitegemea kufanya shughuli hii ya uchimbaji kwa ufanisi.
Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Chunya umekimbizwa umbali wa kilometa 287.4 na miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni mia nane imezinduliwa, kutembelewa na miradi mingine kuwekewa mawe ya msingi.
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya jamii, Bi Marietha Mlozi akisoma taarifa ya mpango maalum wa urasimishaji wa wachimbaji wa dogo kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2024 ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava
kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 kitaifa ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava akipokea taarifa ya mpango maalum wa urasimishaji wachimbaji wadogo kutoka kwa Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii bi Marietha Mlozi Wilayani Chunya wakati wa Mkesha wa Mwenge wa Uhuru .
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.