Gharama kubwa za uchimbaji wa visima vya maji kupitia mitambo ya serikali iliyonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwarahisishia wananchi kupata maji zimetua Bungeni leo kupitia Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njelu Kasaka baada ya kuhoji ukubwa wa Gharama ya kutumia mitambo hiyo ukilinganisha na Mitambo Binafsi ya uchimbaji wa visima wilayani Chunya
Mhe Masache ameiuliza serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo 8/11/2023 katika bunge linaloendela jiji Dodoma kwamba uchimbaji wa Maji kupitia mitambo ya serikali imekuwa na gharama kubwa kuliko mitambo ya Taasisi Binafsi suala ambalo sio lengo la Serikali huku akiitaka serikali kutazama upya bei hizo ili lengo la Serikali inayoongozwa Na Mhe Dkt Samia suluhu Hassan la kumtua Mama Ndoo Kichwani litimie wilayani Chunya
“Serikali imekuwa na nia njema kuendela kutatua changamoto ya maji hasa kwenye maeneo yetu na imeweza kununua magari ya kuchimba visima na kuyagawa kwenye mikoa yetu, lakini Changamoto ni gharama kubwa ambayo inajitokeza pale taasisi za serikali zinapotaka kuyatumia magari hayo je ni upi mwongozo wa Serikali unaoelekeza matumizi ya magari haya gharama ziwe chini kuliko wachimbaji Binafsi?” Mhe Masache aliuliza
Naibu waziri wa maji Mhe Maryprisca Mahundi amesema Lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona watu wanatumia mitambo hii kutatua kero ya Maji hivyo serikali itaangalia uwezokano wa bei kupungua kiasi cha Taasisi na wananchi kumudu na hatimaye kuendelea kuitumia mitambo hiyo kutatua changamoto za maji maeneo yao
“Mhe Naibu Spika hizi gharama ni kutokana na ubora wa kazi unaofanywa na wataalam wetu, unaweza kuchimbiwa kwa gharama ndogo na mtu binafsi lakini baada ya muda unaanza kulalamika unapata maji yaliyo chini ya ubora lakini sisi gharama zetu zinaonekana kubwa lakini ubora wa maji na sababu ni kwamba sisi tunaweza kwenda chini mita 200 ndo maana tunakuchaji milioni 20, mtu binafsi anaweza kwenda mita 70 na akakuchaji milioni tano ukaona ni ni rahisi kwahiyo ubora wa maji unaenda kwa kutofautina na hapo ndipo gharama inapokuwa kubwa , lakini kwa kuzingatia Mhe Rais anahitaji kuona magari haya yanaendelea kutumiwa na watu wengi tutaendeleo kuona kadiri tuwezavyo gharama inakuwa rafiki” alijibu Naibu waziri wa Maji Mhe Mahundi
Ikumbukwe hivi karibu Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka katika kikao cha Kawaida cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Chunya alisema Uchimbaji wa Maji kupitia mitambo iliyonunuliwa na Mhe Rais ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania wakiwepo wanachunya imekuwa kubwa kuliko mitambo ya watu binafsi na kuagiza wahusika kufika ofisini kwake kuzungumia suala hilo ili kuona uwezekano wa kupendekeza kwa mamlaka zinazohusika kutazama suala hilo ili mitambo hiyo iwasaidie wananchi wengi zaidi kama ambavyo serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani ilivyokusudia
Kilio hicho cha gharama za kutumia mitambo ya serikali kuchimba visima vya maji kufika Bunge la Jamhuri ya Muunganmo wa Tanzania kupitia mwakilishi wa wanachunya kwenye Bunge hilo inaonesha namna ambavyo viongozi wa wilaya ya Chunya wanavyohangaika kwa pamoja kuhakikisha kero za wananchi wa wilaya ya Chunya zinaptiwa majibu kwa wakati
Bunge linaendelea na vikao vyake vyenye lengo la kujadili ripoti ya Mdhibi na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) na kuanza maandalizi ya Mpango wa Serikali kwaajili ya mwaka wa fedha ujao ambapo wananchi wa wilaya ya Chunya (ambalo ni Jimbo la Uchaguzi la Lupa) wanawakilishwa na Mbunge wa Jimbo hilo la Lupa Mhe Masache Njelu kasaka.
Mbunge wa Jimbo la Lipa Mhe Masache Njelu Kasaka akiuliza swali mapema leo Bungeni kuhusu gharama za uchimbaji wa visima kutumia mitambo ya serikali
Naibu waziri wa Maji Mhe Maryprisca Mahundi akijibu swali la Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa mapema leo
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Kasaka (Wa katikati) akisikiliza kwa makini majibu ya Naibu waziri wa Maji kuhusu kero ya gharama kubwa za kutumia mitamvo ya serikali ya kuchimba maji ukilinganisha na mitambo Binafsi
Picha ikionesha Bunge la Jamhuri ya Munngano wa Tanzania likiendelea na shughuli zake Jijini Dodoma mapema leo
Mitambo (Magari) yanayolalamikiwa kutoza gharama kubwa katika uchimbaji wa visima vya maji ukilinganisha na mitambo au magari Binafsi kwa Mkoa wa Mbeya mitambo hii iko wilayani Chunya kwa sasa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.