Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh. MAYEKA SIMON MAYEKA amewataka wananchi waliojitokeza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria kutofumbia macho kesi za ubakaji na ulawiti kwakuwa zinaathari mbaya kwa jamii kwani athari zake zinadumu kwa muda mrefu
Mayeka ametoa kauli hiyo (jana) katika kilele cha hitimisho ya wiki la sheria wilayani Chunya hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi na maewaonya viongozi na wananchi waliojitokeza kuepuka maelewano katika kesi za ulawiti na ubakaji kwani zina athari kubwa kwa jamii
“Msitake maelewano katika kesi za namna hii, mtoe ushirkiano mapema, tuchukue hatua mapema ili haki itendeke. Hasa viongozi wetu wa vijiji wanashawishika kufanya mazungumzo na mara nyingi ni pale aliyefanya ni ndugu”
Aidha Mayeka ameendelea kuhimiza jamii kukataa, kupinga na kuzuia mila na maadili potofu kuwafikia watoto wetu kwa nguvu zetu zote kwani kinyume na hapo siku zijazo tutakuwa na Taifa la hovyo, lisilo na maadili, Hivyo ni jukumun letu sote kuhakikisha tunalinda maadili yetu kama nchi
Katika kuhitimisha hotuba yake Mayeka ameendelea kuhimiza wazazi na walezi wote wilayani Chunya kuhakikisha watoto waliochaguliwa kujiunga na masomo katika shule za sekondari wapelekwe shule, huku akiwataka Mahakimu kuendelea kuwashughulikia wazazi wanaogoma kuwapatia watoto haki za msingi ikiwepo kuwapatia elimu
Awali akitoa taarifa Mbele ya Mgeni rasmi Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Chunya James Julius Mhanusi amesema katika maadhimisho ya wiki ya sheria wilayani chunya wamefanya shughuli mbalimbali ikiwepo kutoa elimu katika shule mbalimbali za sekondari na msingi zilizopo wilayani Chunya pia wametembelea wananchi katika kata mbalimbali ili kuwapelekea elimu ya sheria za nchi
Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya chunya amesema kasi ya usikilizaji wa kesi wilayani chunya ni mzuri kwani kesi nyingi zimepatiwa ufumbuzi kwa wakati hivyo kuwarahisishia wananchi kwanza kuepukana na gharama za kufika mahakamani mara kwa mara lakini pia kumaliza kesi kwa wakati kunasaidia wananchi kupata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali
Mhanusi ameongeza kuwa Mahakama ya wilaya ya Chunya pamoja na uwepo wa hakimu mmoja wa mahakama hiyo lakini imesikiliza zaidi ya mashauri 464 kati ya mashauri 560 ambapo mashauri yaliyofunguliwa mwaka 2022 na yale machache ambayo walivuka nayo mwaka 2021.
Kwakuhitimisha hotuba yake mbela ya Mgeni rasmi, Hakimu mkazi mfawidhi amewataka wadau wote wa mahakama wilayani chunya kuendelea kuwa na Imani na mahakama zote wilayani humo kwani wao wataendelea kutekeleza jukumu lao kikamilifu kila wakati
Maadhimisho ya wiki ya sheria wilayani chunya yamefanyika kuanzia tarehe 22/01/2023 mpaka tarehe 29/01/2023 ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika katika maeneo tofauti tofauti ndani ya wilaya huku kilele chake kikiwa ni tarehe 01/02/2023, Kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya Sheria mwaka 2023 ni “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endekevu; Wajibu wa Mahakama na wa
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.