Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Juma Aweso amesema ndani ya wiki MOJA milioni miatano italetwa mbeya ili kutatua changamoto ya maji katika kijiji cha Itumbi na Mwala ikiwa ni kuendelaza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025, ifikapo 2025 wananchi waishio vijijini wapate maji kwa asilimia themanini na tano (85%) tofauti na ilivyosasa ambapo wananchi vijijini wanapata maji kwa asilimia sitini na tatu (63)
Mhe: Aweso amesema hayo jana tarehe 11/2/2023 katika hafla ya utiliaji saini mkataba wa ujenzi mradi wa maji kutoka mto Kiwira iliyofanyika Jijini Mbeya katika viwanja vya shule ya Msingi Hasanga Mkabala na mizani uyole, Mradi ambao unataraji kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 117 ambapo maji lita milioni 180 zitazalishwa kwa siku wakati mahitaji kwa sasa ni lita milioni tisini (90)
“Nimepata maombi kutoka kwa mkuu wa Mkoa, nimepenyezewa maombi na spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia nimepata maombi kutoka kwa Naibu waziri wa Maji kwamba kuna changamoto kubwa ya Maji Itumbi, Mheshimiwa Naibu waziri wa Maji tukitoka hapa tukafanya mawasiliano na katibu mkuu wizara ya maji ili ndani ya wiki moja, shilingi milioni mitano (500) zije mbeya kutatua kero ya Maji katika kijiji cha Itumbi na Mwala”
Aidha Mhe Aweso amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu hassan amesema niwaambie kwamba ahadi zote alizowaahidi wanambeya atazitekeleza na amesema anawapenda sana wana mbeya na anawaamini sana.
Maelezo mahususi aliyonipatia kwa wana mbeya ni haya; Rais ameniagiza niwambie wana Mbeya kwamba ahadi zote alizoziahidi kwa wana Mbeya atazitekeleza”
Sambamba na hilo Mhe Aweso amsema Rais Samia na serikali anayoiongoza imeadhimia kumtua ndoo Mama kichwa hivyo imenunua gari (mtambo) la kuchimbia visima vya maji kwa mikoa yote ya Tanzania na amemwagiza Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji kuhakikisha anakabidhi gari hiyo kwa Mkuu wa Mkoa ili eneo ambalo kuna shidaa ya Maji basi kuchimbwe visima ili wananchi wasihangaike kupata Maji
“Mhe Spika naomba nikupe salamu za wizara ya Maji na maelekezo ya Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Nchi yetu katika mikoa yote 25 serikali imenunua mitamboi maalumu ya kuchimbia visima vya maji kwa maeneo ambako wananchi hawana maji. Nakuagiza Naibu waziri Kabla haujaondoka Mbeya Wiki hii uwe umekabidhi gari ya kuchimba visima kwa Mkuu wa Mkoa”
Awali akizungumza Mbele ya waziri wa Maji na umwagiliaji, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe; JUMA ZUBERI HOMERA alimweleza waziri uwepo wa Changamoto ya maji katika Kijiji cha Itumbi kilichopo kata ya Matundasi huku ikieleza namna Itumbi inavyochangia katika ukusanyaji wa dhahabu wilayani chunya ambapo Zaidi ya kilogramu 100 hupatikana kwa mwezi kutoka itumbi lakini eneo hilo maji imekuwa tatizo kubwa
“Kuna tatizo moja pale Itumbi wilayani chunya, Pale Itumbi wanazlisha kilogramu 100 za dhahabu kwa mwezi wanaleta pale chunya lakini wanachangamoto kubwa ya Maji tungeomba mweshimiwa waziri tusaidie pale waweze kupata maji safi na salama ili wachenjue vizuri dhahabu zao waongeze uzalishaji ili walete dhahabu za kutosha kwenye soko la dhahabu tupate fedha zaidi tuendelee kujenga miradi ya maji. Pia kule Mwala iliyoko Mbeya vijijini kuna changamoto kubwa ya Maji. Mweshimiwa waziri ukituletea milioni miatano pale Itumbi na pale Mwala milioni 500 kazi inaisha mweshimwa Aweso”
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso(Mgeni rasmi) spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe Dkt Tulia Ackson Mwansasu, Mhe Oran Njeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini na Mwenyekiti wa wabunge wote mkoa wa Mbeya na viongozi wengine wakati wilaya ya Chunya Ikiongozwa na Afisa Tarafa Tarafa ya kiwanja Erick F.Nyoni akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka Simon Mayeka akiambana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu TAMIMU KAMBONA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona akiwa kwenye Hafla ya Utiaji saini mkataba wa Ujenzi wa mradi wa maji kutoka mto Kiwira iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Hasanga Jijini Mbeya
|
|
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.